AMKA NA BWANA LEO 02/06/2022

TENDA WEMA KATIKA KAZI YAKO SI KANISANI TU

Basi yoyote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo torati na manabii. Mathayo 7:12.

📚 Wale ambao kweli wanamcha Mungu ni bora wafanye kazi mchana na usiku, na kula mkate wa umasikini, kuliko kuendekeza shauku za kujipatia mali ambazo zitawagandamiza wajane na yatima, au kuwanyima wageni haki zao. Mkombozi wetu alitaka kuwahimiza wasikilizaji Wake kwamba mtu ambaye angejitosa kumtapeli jirani hata kwa kitu kidogo kabisa, angewarubuni kwa mambo makubwa kama nafasi ingeruhusu. Kuchepuka kidogo tu kutoka kwenye uadilifu kunavunja vizuizi, na kuuandaa moyo kufanya udhalimu mkubwa. Kwa kanuni na mifano Kristo alifundisha kuwa uadilifu halisi unapaswa kutawala mwenendo wetu kwa wenzetu. Mwalimu wa mbinguni alisema, "Basi yoyote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo."

📚 Kwa kiwango ambacho watu wangejinufaisha kwa hasara ya wengine roho zao vivyo hivyo hawatajali ushawishi wa Roho wa Mungu. Kipato kilichopatikana katika gharama hiyo ni hasara ya kutisha. Ni bora kukosa kuliko kudanganya; ni heri kuwa na njaa kuliko kunyang'anya; ni heri kufa kuliko kufanya dhambi. Ubadhirifu, ulaghai, ujambazi unaoendekezwa na wale wanaokiri utauwa, unaharibu imani yao na unaharibu hali yao ya kiroho. Kanisa linawajibika kwa kiwango kikubwa kwa dhambi za waumini wake. Linatoa mwonekano wa uovu ikiwa linashindwa kupaza sauti yake dhidi yao. Ushawishi ambao linapaswa kuuogopa zaidi sio ule wa wapinzani wa wazi, makafiri na wanaokufuru, bali wa wale wanaomkiri Kristo wasiofuata utaratibu. Hawa ndio wanaozuia baraka za Mungu kwa Israeli....

🔘 Shughuli za kiulimwengu hazipaswi kuwa nje ya mipaka ya serikali ya Mungu. Dini ya kweli haipaswi kuoneshwa tu siku ya Sabato na kuonekana madhabahuni; inapaswa kuonekana kila siku na kila mahali. Madai yake sharti yazingatiwe na kutiiwa katika kila tendo maishani. Wale wenye dini ya kweli wataionesha katika biashara zao zote utambuzi wazi wa haki kama wanavyokuwa wakiwasilisha maombi yao kwenye kiti cha enzi cha neema. The Southern Watchman, May 10, 1904.

MWENYEZI MUNGU AKUBARIKI SANA

No comments