𝐓𝐄𝐓𝐄𝐒𝐈 𝐙𝐀 𝐒𝐎𝐊𝐀 𝐔𝐋𝐀𝐘𝐀 𝐉𝐔𝐌𝐀𝐍𝐍𝐄 28/06/2022
➪Tottenham inataka kumsajili mshambuliaji Richarlison 25, na winga Anthony Gordon , 21 kutoka Everton katika mikataba miwili . Chelsea pia ina hamu ya kumsajili Richarlison.. (Sky Sports)
➪Lakini Everton haina hamu ya kumuuza Gordon ambaye kandarasi yake na klabu hiyo ya Goodison Park inakamilika 2025, ikiwa ni Pamoja na kandarasi yoyote itakayomuhusisha Richarlison.. (Liverpool Echo)
➪Spurs pia wanapigiwa upatu kumsajili beki wa Barcelona na Ufaransa Clement Lenglet, licha ya Roma kuwa nah amu ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27. (London Evening Standard)
➪Kiungo Jude Bellingham, 18, atakuwa mchezaji anayesakwa sana na Real Madrid msimu ujao , licha ya kwamba klabu hiyo ya Hispania inakabiliwa na ushindani kutoka kwa Chelsea na Liverpool. (AS, via Mail)
➪Baada ya kufungua mazungumzo na klabu ya Manchester City kuhusu kumsajili Raheem Sterling ,27 Chelsea inajaribu kumsajili beki wa Uholanzi 27 kutoka kwa mabingwa hao wa ligi ya kuu ya Premia.. (Telegraph - subscription required)
➪Arsenal wamewasilisha ofa ya pauni milioni 35 kwa mlinzi wa Ajax Lisandro Martinez na wanaonekana kuiongoza Manchester United katika kinyang'anyiro cha kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina, 24. (Kioo)
➪Manchester United wanatumai kuhitimisha kandarasi za kiungo wa kati wa Barcelona na Uholanzi Frenkie de Jong, 25, na kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen, 30, na kisha wataelekeza umakini wao kumsaka mshambuliaji, huku Mbrazil wa Ajax Antony, 22, akiwa lengo lao kuu.
➪Mkataba wa kumnunua Antony umewekwa shakani huku Ajax sasa ikitaka pauni milioni 70 kumnunua fowadi huyo. (Kioo)
➪Newcastle United wanatazamia kukamilisha usajili wa pauni milioni 32 wa mlinzi wa Lille Sven Botman, 22, lakini wako tayari kuendelea na harakati zao za kumnunua mshambuliaji wa Reims Mfaransa Hugo Ekitike, 20. (Mail).
TANGAZA NASI KWA GHARAMA NAFUU, TUPIGIE 0621663340
Post a Comment