𝐓𝐄𝐓𝐄𝐒𝐈 𝐙𝐀 𝐒𝐎𝐊𝐀 𝐔𝐋𝐀𝐘𝐀 𝐉𝐔𝐌𝐀𝐓𝐀𝐓𝐔 20/06/2022:

 

➪Tottenham wana matumaini ya kuwapiku mahasimu wao wa kaskazini mwa London Arsenal  katika mbio za kumsaka  mshambuliaji wa Manchester City  Mbrazili Gabriel Jesus kwa ofay ya  soka ya Championi Ligi   . (Mirror)


➪Mshambuliaji wa Manchester City na England  Raheem Sterling, 27, amekuwa akiwauliza watu kuhusu maisha katika magharibi mwa London huku klabu ya Chelsea ikiwa na nia naye. (Athletic)


➪Dau la awali la £21.5m kwa ajili ya Sterling limekataliwa. (Fabrizio Romano)


➪Chelsea wanaweza pia kumuhitaji  mlinzi wa Manchester City mwenye umri wa miaka 27- Mholanz Nathan Ake. (Telegraph, subscription required)


➪Mshambuliaji wa Chelsea na Ubelgiji  Romelu Lukaku, 29, yuko tayari kurejea katika Inter Milan kwa gharama ya mkopo wa £8.5m pamoja na marupurupu aliyokubaliwabaina ya klabu hizo. (Mail)


➪Manchester United  wanaangalia uwezekano wa kufanya dai jipya kwa ajili ya kiungo wa kati wa Barcelona na Uholanzi mwenye umri wa miaka 25 Frenkie de Jong. (Fabrizio Romano)


➪Kiungo wa kati wa Wolves na Ureno Ruben Neves, 25, yuko katika orordha ya Manchester United ya wachezaji inayoweza kusaini mkataba nao iwapo watashindwa kusaini mkataba na De Jong. (Fabrizio Romano, via givemesport)


➪Newcastle wamepewa ofay a fursa ya kusiani mkataba na mlinzi Mivory Coast Eric Bailly, 28, kutoka Manchester United. (Mirror)


➪The Magpies pia wameambiwa kuwa ni lazima walipe  £50m kusaini mkataba na winga wa  Bayer Leverkusen  na Ufaransa Moussa Diaby. (Sun)


➪Nyota wa Ureno Cristiano Ronaldo, 37, ameafiki haja ya Manchester United ya kusaini mkataba na mshambuliaji mpya. (Express)


➪Meneja wa Uholanzi  na meneja wa zamani wa  Manchester United boss Louis van Gaal alihusika kwa sehemu katika kumzuwia mlinzi wa Ajax  Mholanzi  Jurrien Timber, 21, kuhamia Old Trafford. (Marcel van der Kraan, Sky Sports)

Tangaza nasi kupitia mitandao ya kijamii, website na App yetu kwa gharama nafuu, tupigie 0621663340


No comments