Ricketts Family imejitoa katika mbio za kuinunua klabu ya Chelsea.
🚨Habari za hivi punde ni kwamba Ricketts Family imejitoa katika mbio za kuinunua klabu ya Chelsea. Familia hii ambayo ilikua ikifanya kazi na mfanyabiashara wa Kimarekani Ken Griffin na Dan Gilbert walikua miongoni mwa matajiri Wanne waliokuwa wanapewa nafasi kuinunua klabu hii.
Akiwemo Sir Martin Broughton, Todd Behly na Stephen Pagliuca ambao bado wapo kwenye kinyang'anyiro cha kuinunua klabu.
Tom na Raula Ricketts ni wamiliki wa wa klabu ya Chicago Cubs baseball. Mwisho wa wamiliki waliobaki kutuma mapendekezo yao ya mwisho kwa Raine Group,ambao wanasimamia shughuli nzima ya kuuzwa klabu ilikua ni Alhamis ila Ricketts Wanasema hawakutuma hayo mapendekezo.
Wiki kadhaa zilizopita mashabiki wa Chelsea waliandamana nje ya uwanja wa Stamford Bridge kupinga familia hiyo kumiliki klabu kwa tuhuma za ubaguzi dhidi wa Waislam.
Na leo ndio siku ya mwisho ya kupokea ofa za kuiuza Chelsea.
🇺🇸🇺🇸🇺🇸🇺🇸
Post a Comment