Povu la kocha wa Orlando Pirates kabla na baada ya Mchezo dhidi ya Simba sc
Kocha wa klabu ya Orlando Pirates 🇿🇦 Mandla Nsikazi ameilalamikia klabu ya Simba sc kwa kuwapa pikipiki moja ya ESCORT katika jiji lililo na harakati nyingi na kupelekea kupata tabu njiani.
.
.
Amesema mambo hayo watalipa nchini kwao South Africa 🇿🇦
Baada ya Mchezo wao pia akatoa malalamiko haya;
"Media zenu zote hapa zinaenda kudanganya na kuandika uongo, semeni ukweli, Simba hakustahili kushinda"
"Simba wamebebwa, hawajatutreat vizuri tangu tumefika, penati waliyopewa hawakustahili, VAR imewekwa lakini haijatumika katika maamuzi"
"Kwa mliyotufanyia tukiwa hapa, je mtafurahi tukiwafanyia mkija South Africa ? Sisi hatutawalipiza tutakuwa waungwana"
🔍 Mcikazi kocha wa Orlando Pirates akiongea kwa ukali na wanahabari.
Post a Comment