Msamaha ndio ulinikasirisha zaidi
Licha ya nyota wa Man Utd Cristiano Ronaldo kuomba msahama kwa kitendo cha kuibamiza chini simu ya bwana Mdogo Jake (14) wakati wa mchezo wa EPL dhidi ya Everton, mama wa mtoto huyo Sarah Kelly aukosoa msamaha huo
"Msamaha ndio ulinikasirisha zaidi, unamwambia kila mtu kwamba umeomba msamaha wakati hujaomba? Sawa, umeweka kwenye mitandao ya kijamii lakini hukupaswa kufanya vile, unapaswa kumuomba msamaha mwanangu"
"Yeye [Ronaldo] alikuwa na masaa kadhaa ya kutafakari juu yake, alitakiwa apate mawasiliano yetu ili azungumze na sisi na kutoa chochote ningefurahishwa na hilo"
"Kiufupi Kulikuwa na watu wengine wengi wakipunga simu zao pande zote, mwanangu alikuwa katika ulimwengu wa kipekee, alikuwa anafurahia ushindi wetu, wakati Ronaldo anatoka uwanjani, mwanangu akasema "Mama, Ronaldo anaumia, ngoja nimrekodi video.' Nikamwambia, 'Sawa'.
" Sikufikiria chochote juu yake, nakumbuka wakati huo alikuwa hamuangalii Ronaldo tena, badala yake alikuwa akiangalia anachokifanya kwenye simu, Ghafla nikashtuka simu ipo chini, mwanangu akaendelea kushangaa"
"Ilikuwa Ni ngumu sana kwangu kuliamini hilo kwasababu, Ronaldo alijua kuwa sehemu ile kuna watoto wengi na ndio maana kabla ya mechi alikuwa akipeana mikono na hao watoto, mechi ilivyoisha ikawa hadithi tofauti kabisa kwa sababu walikuwa wamepoteza, anachotakiwa kujua mpira hauko hivyo, Huwezi kushinda kila siku"
"Najua Kama mtu akikufanyia hivyo mtaani anakamatwa na kuhojiwa, nina uhakika hata kama angekuwa mtu mwingine ambaye amempeleka mtoto wake kwenye mechi hiyo na kukutana na hali hiyo angefadhaika sana na kushtuka pia"
KUHUSU MWALIKO WA RONALDO OLD TRAFFORD
"Nilimuuliza Mwanangu Je, ungependa kwenda kwasababu Ronaldo ametualika, Akasema, 'Hapana, mama, sitataka kumuona tena" Alizungumza Sarah kupitia Telegraph Sports
Ikumbukwe kuwa Polisi wa Merseyside wanatarajia kupitia picha za CCTV ili kubaini kama Cristiano Ronaldo alitenda kosa la kunyang'anya na kubamiza chini simu ya shabiki huyo kabla hawajachukua hatua zaidi.
Post a Comment