AMKA NA BWANA LEO 26/04/2022
*ELIMU YA KWELI YA JUU INAPATIKANA KATIKA NENO LA MUNGU*
*Jipatie hekima, jipatie ufahamu; usiusahau; wala usiyakatae maneno ya kinywa changu*.
*Mithali 4:5*
Hakuna muda sasa wa kujaza akili kwa dhana za uongo ambayo inaitwa elimu ya juu. *Hakuwezi kuwa na elimu ya juu zaidi ya ile ijayo kutoka kwa Mwandishi wa ukweli. Tunapaswa kulichunguza Neno la Mungu. Inatulazimu kuwaelimisha watoto wetu katika kweli zipatikanazo humo. Ni hazina isiyokwisha*; lakini wanaume na wanawake wanashindwa kupata hazina hii kwa sababu hawaitafuti mpaka iwe ndani ya umiliki wao. *Katika Neno hili kunapatikana hekima, hekima isiyo na shaka na isiyo na mwisho, ambayo haikutokana na akili zenye ukomo, bali katika akili isiyo na mwisho*.
Wakati wanaume na wanawake wanapokuwa tayari kufundishwa kama watoto wadogo, wanapo jisalimisha kabisa kwa Mungu, watapata katika Maandiko sayansi ya elimu. *Wakati walimu na wanafunzi wanapoingia katika shule ya Kristo, wajifunze kutoka kwake, watazungumza kwa busara juu ya elimu ya juu, kwa sababu wataelewa kwamba ni elimu hiyo ambayo inawawezesha watu kuelewa kiini cha sayansi.*
*Wale watakaotafuta kwa mafanikio hazina iliyositirika lazima ainuke kwa shughuli za juu kuliko vitu vya ulimwengu huu. Mapenzi yao na uwezo wao lazima yawekwe wakfu katika utafiti huu*. Wanaume na wanawake wa uchaji na talanta hupata maoni ya ukweli wa milele, lakini mara nyingi wanashindwa kuelewa, kwa sababu mambo yale yanayoonekana yanazuia utukufu wa yale yasiyoonekana. *Kwa wengi hekima ya wanadamu inafikiriwa kuwa juu kuliko hekima ya Mwalimu wa uungu, na kitabu cha kufundishia cha Mungu kinatazamwa kama kilichopitwa na wakati, kiasi kwamba kinaweza kufikiriwa kuwa dhaifu na kisichofaa. Bali kwa wale ambao wamehuishwa na Roho Mtakatifu halichukuliwi hivyo. Wanaona hazina isiyokadirika, na wangeuza kila kitu ili kununua shamba mahali ilipo*.
*Wale wanaojifunza Neno la Mungu, wanaochimba kwa ajili ya hazina za ukweli, watathamini kanuni nzito zinazofundishwa humo, na watazichimba ndani zaidi. Kama matokeo, watajazwa na Roho wa Kristo; na kwa kutazama, watabadilishwa wafanane naye. Watafundisha kama wanafunzi ambao wamekuwa wakikaa katika miguu ya Yesu, ambao wamezoea kujifunza kutoka kwake, ili kwamba waweze kumjua Yeye ambaye kumjua vyema ni uzima wa milele.*
*MWENYEZI MUNGU ATUBARIKI TUNAPOTAFAKARI NENO LAKE*
Post a Comment