AMKA NA BWANA LEO 23/03/20222

KESHA LA ASUBUHI 

JUMATANO, MACHI 23 2022

WATUMIAJI WAAMINIFU WA TALANTA WATASIKIA “VYEMA SANA”

Mara yule aliyepokea talanta tano akaenda, akafanya biashara nazo, akachuma faida talanta nyingine tano. Vile vile na yule mwenye mbili, yeye naye akachuma nyingine mbili faida. Mathayo 25:16, 17.

▶️ "Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele." Fedha ya fidia imeshalipwa kwa ajili ya kila kijana na binti wa Adamu, na [ukweli] kwamba wale ambao wamelipiwa fidia kwa damu ya thamani ya Kristo wanakataa kumtii hautawafunika dhidi ya adhabu ambayo itawajia katika siku ya mwisho. Watakuwa hawana jibu kwa kupuuza kwao kutumia talanta walizopewa kwa ajili ya Bwana. Watalazimika kujibu kwa ukengeufu wao dhidi ya Muumbaji na Mkombozi wao, kwa unyang'anyi wao kwa Mungu kwa kuzuia talanta zao katika huduma Yake, na kuzika mali za Bwana wao ardhini.

▶️ Familia ya kibinadamu imeundwa na mawakala wawajibikaji wa maadili, na kutoka kwa wenye vipawa vya juu zaidi hadi wa chini zaidi na wasioonekana, wote wamewekezewa amana za mbinguni. Wakati ni karama iliyotolewa ya Mungu, na unapaswa kutumiwa kwa bidii katika huduma ya Kristo. Mvuto ni karama ya Mungu, na unapaswa kutumiwa kwa kupeleka mbele makusudi ya juu na ya uadilifu mkubwa. Yesu Kristo alikufa juu ya msalaba wa Kalwari ili kwamba mvuto wetu wote uweze kutumiwa kumwinua juu mbele ya ulimwengu unaopotea. Wale wanaomtazama Mwalimu wa mbinguni akifa katika msalaba kwa ajili ya uovu wao watathamini mvuto wao pale tu utakapokuwa ukivuta wanaume na wanawake kwa Kristo, na watautumia kwa kusudi hili peke yake. Akili ni talanta iliyotolewa. Huruma na upendo ni karama zinazopaswa kuongozwa na kuboreshwa kwa heshima sana, ili kwamba tuweze kumtolea huduma Yeye ambaye sisi tulinunuliwa kwa mali Yake.

🔘 Vile jinsi tulivyo au tutakavyokuwa tu wake Mungu. Elimu, nidhamu, na ujuzi katika kila sehemu vinapaswa kutumiwa kwa ajili Yake.... Iwe ni kiasi kikubwa au kidogo kilichotolewa, Bwana anahitaji kwamba wenye nyumba Wake wafanye bidii. Sio kiasi kilichotolewa au uboreshaji uliofanywa utakaowaleta wanaume na wanawake kibali cha mbingu, bali uaminifu, utii kwa Mungu, huduma ya upendo iliyotolewa, ambavyo huleta baraka za Mungu "Vyema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya Bwana wako." Zawadi hii ya furaha haisubiri mpaka kuingia kwetu katika Jiji la Mungu, bali mtumishi mwaminifu ana limbuko la furaha hiyo hata katika maisha haya.

MWENYEZI MUNGU AKUBARIKI SANA

No comments