AMKA NA BWANA LEO 21/03/2022
JUMATATU, MACHI 21 2022
KUFANYA KAZI NA YESU KUOKOA WALIOPOTEA
Tazama, Naja upesi, na ujira Wangu u pamoja Nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. Ufunuo 22:12.
📚 Bwana Yesu atachunguza kwa makini kila talanta, na kutegemea faida kulingana na kiasi cha mtaji kilichotolewa. Kwa kufedheheshwa na uchungu Wake mwenyewe, Kristo alilipia thamani ya gharama ya wokovu wetu, na anayo haki ya huduma zetu. Jina lenyewe la mtumishi linadokeza ufanyaji wa kazi, ubebaji wa jukumu. Uwezo wetu wote, fursa zetu zote, zimekabidhiwa kwetu kwa maboresho ya busara, ili kwamba Kristo apokee iliyo Yake na riba.
📚 Mwalimu wa mbinguni alipaa juu, na aliteka mateka, na alitoa karama kwa wanaume na wanawake—hazina za uungu za ukweli ili ziwasilishwe kwa ulimwengu wote. Je! Ni matumizi gani tunayoyafanya binafsi kwa zawadi hizi, talanta hizi zilizoko mikononi mwetu? Je! Sisi tu kama mtumwa mlegevu na asiye mwaminifu, tukizika karama hizi katika ulimwengu, ambapo hazitaleta faida kwa Mungu? Inastahili wote kwa uaminifu makini kuboresha talanta walizokabidhiwa; kwa kuwa talanta zitakua pale zinapotumiwa kwa faida ya wanadamu na kwa utukufu wa Mungu.
🔘 Kila nafsi inapaswa kutafuta kwanza ufalme wa Mungu na haki Yake. Hatupaswi kutumia kabisa nguvu za ubongo, mifupa, na misuli katika shughuli zenye faida kwa ulimwengu; kwa kuwa kama tukifanya, tunahatarisha faida zetu za kiroho, na tutapoteza furaha ya Milele. Ulimwengu wote usioanguka una shauku katika kazi kubwa ambayo Yesu Kristo alikuja katika ulimwengu wetu kuikamilisha, haswa wokovu wa nafsi zetu. Na je! Wanadamu walio na ukomo duniani hawatashirikiana na Mkombozi wetu, ambaye alipaa kwenda mbinguni kufanya maombezi kwa ajili yetu? Je, tusioneshe juhudi maalumu, wala kupenda kujitolea, katika kazi ambayo ilibuniwa mbinguni kupelekwa ulimwenguni kwa ajili ya faida ya wanaume na wanawake? Je, sisi ambao tumenunuliwa kwa damu ya thamani ya Kristo tukatae kuifanya kazi tuliyowekewa mikononi mwetu tukatae kushirikiana na mawakala wa mbinguni katika kazi ya kuokoa walioanguka? Je, tusiende hata miisho kuifanya nuru ya mbinguni ya Ukweli tuliopewa ing'ae kwa wanadamu wenzetu?
MUNGU AKUBARIKI SANA
Post a Comment