Ahmed Ally on SimbaSC vs RS Berkane next Sunday " they will suffer"
𝐖𝐀𝐓𝐀𝐕𝐔𝐓𝐀 𝐏𝐔𝐌𝐙𝐈 𝐘𝐀 𝐌𝐎𝐓𝐎
➪“Watavuta pumzi ya Moto, pumzi ambayo wanasimba tumeshaizoea, kama tuliweza kuwadhibiti kwao wakaja kuamua matokeo kwa mipira iliyokufa basi moja Kwa moja tunaweza kuwadhibiti hapa,”
𝐓𝐔𝐍𝐀 𝐂𝐇𝐀𝐍𝐆𝐀𝐌𝐎𝐓𝐎 𝐘𝐀 𝐊𝐔𝐔𝐙𝐀 𝐓𝐈𝐊𝐄𝐓 𝐒𝐈𝐊𝐔 𝐘𝐀 𝐌𝐄𝐂𝐇𝐈
➪“Tuna changamoto kubwa ya kununua tiketi siku ya mchezo, tuna changamoto ya kununua tiketi uwanjani hii inatusumbua sana, mfano mechi iliyopita dhidi ya ASEC Mimosas hadi kufika siku moja kabla ya mchezo tuliuza tiketi elfu kumi (10,000)…
𝐖𝐀𝐒𝐇𝐀𝐁𝐈𝐊𝐈 35,000 𝐒𝐈𝐌𝐁𝐀 𝐕𝐒 𝐑𝐒 𝐁𝐄𝐑𝐊𝐀𝐍𝐄
➪“Kwa maelekezo ya CAF idadi ya washabiki imeruhusiwa ile ile ambayo iliruhusiwa kwenye mechi dhidi ya ASEC Mimosas Kwa maana ya washabiki 35,000, tuliomba idadi iwe 60,000 yaani uwanja mzima lakini CAF wameturuhusu hao 35,000,”
𝐃𝐈𝐋𝐔𝐍𝐆𝐀 , 𝐂𝐇𝐀𝐌𝐀 𝐖𝐀𝐓𝐀𝐊𝐎𝐒𝐄𝐊𝐀𝐍𝐀
➪“Chama hatokuwepo kwenye mchezo dhidi ya RS Berkane kutokana na Kanuni na hiyo wanasimba wote wanafahamu, lakini Hassan Dilunga naye tutamkosa yeye bado Afya yake haijakaa vizuri tangu ameumia mguu anaendelea na matibabu lakini sehemu kubwa ya nyota wetu wamerejea,”
“Hali ya hewa ya Dar es Salaam tunaitumia kama advantage, RS Berkane watapata tabu kwenye joto la Dar es Salaam, kwenye jua la Dar es Salaam tuna uhakika watapata tabu,” Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba SC Tanzania Ahmed Ally ndani ya Sport Arena.
Post a Comment