POLAND KUKATAA KUCHEZA NA URUSI - KUFUZU KOMBE LA DUNIA


Rais wa shirikisho la soka la Poland, Cezary Kulesza ameeleza kuwa timu ya taifa lake haitakuwa tayari kucheza mchezo wa kuwania kufuzu kucheza kombe la Dunia ( WC play off ) vs Urusi kutokana na uvamizi ambao Urusi wamefanya dhidi ya taifa la Ukraine.
.
Mshindi wa mchezo huo anatakiwa kucheza na kati ya Sweden au Czech lakini hata hivyo rais huyo amesema wako ktk mazungumzo na mashirikisho ya nchi hizo ili nao kuweka msimamo huo.
.
LEWANDOWSKI ANENA :
.
Kwa upande wa nyota wa Poland, Robert Lewandowski amesema :
- “ ni uamuzi sahihi! sipati picha eti kucheza na timu ya Taifa ya Urusi wakati majeshi yao yanaendelea kuvamia Ukraine. Wachezaji wa Urusi na mashabiki tunajua hawahusiki na hili lakini hatuwezi kuishi kama vile hakuna kitu kinachoendelea.” #binagotvapp 

Kwa habari za SOKA na BURUDANI tembelea Binago TV  kila wakati hakika hutopitwa na chochote saa 24

#worldcup #UkraineCrisis

No comments