MPIMA ARDHI WA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA PAMOJA NA AFISA MIPANGO MJI KATIKA MKOA WA SHINYANGA WAFARIKI DUNIA

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Imesikitika kutangaza kifo cha mtumishi Johachim E. Henjewele aliyekuwa Afisa Mipango Miji katika Mkoa wa Shinyanga.

Msiba umetokea 18/02/2022 katika Hospitali ya Bugando na taratibu za mazishi zinaendelea.

Pia Wizara hiyo, Imetangaza kifo cha mtumishi Suddy Maulid aliyekuwa Mpima Ardhi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga.

Msiba huo umetokea Tarehe 18/02/2022 saa 5.15 usiku katika Hospitali ya Bombo na taratibu za mazishi zinaendelea.

#RIP...🙏

No comments