AMKA NA BWANA LEO 27/02/2022

JUMAPILI, FEBRUARI 27 2022

*UTII UNA THAWABU ZA HIVI PUNDE NA ZA MILELE*
 
*Kwa hiyo yawekeni maneno Yangu mioyoni mwenu na rohoni mwenu; yafungeni yawe dalili juu ya mikono yenu, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yenu. Kumbukumbu la Torati 11:18.*

Maneno haya [Kumbukumbu la Torati 11:13-28 na 7:6-11] yanapaswa kuwekwa muhuri kabisa katika kila nafsi kama yaliyoandikwa kwa kalamu ya chuma. *Utii unaleta thawabu yake, kutotii adhabu yake.*

*Mungu amewapatia watu wake maagizo chanya, na ameweka juu yao makatazo chanya, ili kwamba waweze kupata uzoefu mkamilifu* katika huduma yake, na kufanywa wafae kusimama mbele za ulimwengu wa mbinguni na mbele za ulimwengu ulioanguka kama washindi. Wanapaswa kushinda kwa damu ya Mwanakondoo na neno la ushuhuda wao. Wale ambao wanashindwa kufanya maandalizi muhimu watahesabiwa pamoja na wasio na shukurani na wasio watakatifu.

*Bwana anawarudisha watu Wake kwa njia ambazo hawazijui, ili kwamba awajaribu na kuwathibitisha. Ulimwengu huu ni mahali pa kuthibitishwa kwetu. Hapa tunaamua hatima yetu ya milele. *Mungu anawanyenyekeza watu Wake ili kwamba mapenzi Yake yaweze kufanywa kupitia wao*. Hivi ndivyo alivyoshughulika na wana wa Israeli alipokuwa akiwaongoza kupitia jangwani. *Aliwaambia vile ambavyo majaliwa yao yangekuwa kama asingelikuwa ameweka mkono Wake kuzuia juu ya kile ambacho kingekuwa kimewadhuru.*

*Mungu anaibariki kazi ya mikono ya wanadamu ili kwamba waweze kurudisha Kwake sehemu Yake.* Wanapaswa kuzisalimisha nyenzo zao kwa huduma Yake, ili kwamba shamba Lake la mizabibu haliwezi kubaki ovyo lisilozaa. Wanalazimika kujifunza kile ambacho Bwana angejifunza kama angekuwa katika pahali pao. *Wanapaswa kuyapeleka mambo yote magumu Kwake kwa njia ya maombi. Wanalazimika kudhihirisha mapenzi yasiyo na ubinafsi katika kuiimarisha kazi Yake kwenye maeneo yote ya ulimwengu.*

*Hebu na tukumbuke kuwa tuwatenda kazi pamoja na Mungu. Hatuna hekima ya kutosha kuweza kufanya kazi peke yetu. Mungu ametufanya sisi mawakili Wake, kutuimarisha na kutujaribu, kama vile alivyowaimarisha na kuwajaribu wana wa Israeli wa zamani. Hatakuwa na jeshi Lake lililotengenezwa na wanajeshi wasio na nidhamu, wasiotakaswa, wapotovu, ambao watawakilisha vibaya mpangilio na usafi Wake.*
*MWENYEZI MUNGU ATUBARIKI TUNAPOTAFAKARI NENO LAKE*

No comments