AMKA NA BWANA LEO 23/02/2022

KESHA LA ASUBUHI 

JUMATANO, FEBRUARI 23 2022

FANYA UTII UVUTIE

Angalieni nawawekea mbele yenu hivi leo baraka na laana; baraka ni hapo mtakaposikiza maagizo ya BWANA, Mungu wenu, niwaagizayo leo; na laana ni hapo msiposikiza maagizo ya BWANA, Mungu wenu, mkikengeuka katika njia niwaagizayo leo, kwa kuandama miungumingine msiyoijua. Kumbukumbu la Torati 11:26-28.

⏯ Wanaume na wanawake hawapaswi kuthubutu kuweka kando viwango vikubwa vya maadili ya Mungu na kusimika viwango kutokana na hukumu zao zenye ukomo. Ni kwa sababu wanajipima wenyewe baina yao wenyewe na kuishi kulingana na viwango vyao wenyewe kiasi kwamba uovu umejaa, na upendo wa watu wengi umepoa. Dharau inaoneshwa kwa sheria ya Mungu, na kwa sababu ya hilo wengi wanathubutu kufanya dhambi, na hata wale ambao waliwahi kupata nuru ya ukweli wanayumba katika utii wao kwa sheria ya Mungu. Je! Mkondo wa uovu ambao umeweka kwa nguvu kuelekea uharibifu utawafyagilia mbali? Au je! Wataweza, kwa ujasiri na uaminifu, kuzuia wimbi na kudumisha uaminifu kwa Mungu katikati ya uovu ulionea?

⏯ Wale ambao wanakiri kumtumikia Mungu wanapaswa kufanya kazi ya kuhuisha wale waliotaabishwa. Wanapaswa kuzaa matunda ya mti mwema. Wale ambao ni wa Kristo kweli kweli hawataleta mateso nyumbani au kanisani. Wazazi ambao wanamfuata Bwana watawafundisha watoto wao kwa uaminifu sheria na amri za Mungu; lakini hawatalifanya hilo katika njia ambayo huduma ya Mungu itakuwa yenye kuchukiza kwa watoto wao. Wazazi watakapo-mpenda Mungu kwa mioyo yao yote, ukweli kama ulivyo katika Yesu utafanyiwa kazi na kufundishwa nyumbani....

🔘 Tunapaswa kujichunguza kwa karibu.... Tunapaswa kumlilia Mungu kutupatia macho ya kiroho, ili tuweze kutambua makosa yetu na kuelewa upungufu wetu wa tabia. Ikiwa tumekuwa wakosoaji na wenye kulaani, tuliojawa na kujawa na kutafuta makosa, kuzungumzia shaka na giza, tunayo kazi ya kutubu na kufanya matengenezo. Tunalazimika kutembea katika nuru, tukiongea maneno ambayo yataleta amani na furaha. Yesu anapaswa kuishi ndani ya nafsi. Na popote alipo, badala ya huzuni, manung'uniko, na kuona uchungu, kutakuwa na tabia ya kupendeza.
MWENYEZI MUNGU AKUBARIKI SANA

No comments