AMKA NA BWANA LEO 15/02/2023

KESHA LA ASUBUHI 

JUMANNE, FEBRUARI 15 2022

FURAHA KATIKA KUPENDA UTII 

Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile ulipoumbwa, hata uovu ulipoonekana ndani yako.... Kwa wingi wa uchuuzi wako watu walikujaza udhalimu ndani yako, nawe umetenda dhambi. Ezekieli 28:15, 16.

▶️ Ili mradi viumbe vyote vilivyoumbwa vilikubali utii wa upendo. kulikuwa na maelewano kamili katika ulimwengu wote wa Mungu. Ilikuwa ni furaha ya wakazi wa mbinguni kutimiliza kusudi la Mwumbaji wao. Walifurahia kuakisi utukufu Wake na kuonesha sifa Zake. Na wakati upendo kwa Mungu ulikuwa wa juu sana, upendo kwa kila mtu na mwenziwe ulikuwa wa kweli na usio na ubinafsi. Hakukuwa na utambuzi wa mafarakano kuharibu amani ya mbinguni. Lakini badiliko lilikuja juu ya hali hii ya furaha.

▶️ Kulikuwa na moja ambaye alipotosha uhuru ambao Mungu alikuwa ameutoa kwa viumbe Vyake. Dhambi ilitokana na yeye ambaye, alimfuatia Kristo, alikuwa ameheshimiwa sana na Mungu na alikuwa na nguvu nyingi zaidi na utukufu kati ya wenyeji wa mbinguni. Lusifa "mwana wa asubuhi," alikuwa kerubi afunikae wa kwanza, mtakatifu na bila unajisi. Alisimama mbele ya Mwumbaji mkuu, na miale isiyokoma ya utukufu iliyomfunika Mungu wa milele ilikaa juu yake....

▶️ Kidogo kidogo Lusifa alianza kuendekeza shauku ya kujitukuza.... Ingawa utukufu wake wote ulitoka kwa Mungu, malaika huyu hodari alianza kuona kuwa ulifungamana na yeye mwenyewe. Hakuridhishwa na nafasi yake, japokuwa alikuwa ameheshimiwa kuliko jeshi la mbinguni, alijitosa kutamani ibada ambayo ilikuwa ya Mwumbaji peke yake. Badala ya kutafuta kumfanya Mungu wa juu zaidi katika mapenzi na utii wa viumbe vyote vilivyoumbwa, ilikuwa jitihada yake kujipatia ibada na uaminifu wao kwake mwenyewe. Na kuutamani utukufu ambao Baba asiye na mwisho alikuwa amemvika Mwanawe, mkuu huyu wa malaika alitaka nguvu ambayo ilikuwa ni haki ya Yesu Kristo pekee. Patriarchs and Prophets, 35.

🔘 Sheria ya upendo ikiwa ndio msingi wa serikali ya Mungu, furaha ya viumbe vyote vyenye akili inategemea makubaliano yao kamili na kanuni zake kuu za haki. Mungu anataka kutoka kwa viumbe Vyake vyote ibada ya upendo-huduma inayotokana na kuithamini tabia Yake. Hafurahishwi na utii uliolazimishwa; na hutoa uhuru wa hiari kwa wote, ili wampatie huduma ya hiari.

MWENYEZI MUNGU AKUBARIKI SANA

No comments