STAA WA WIKI LEO 25/01/2022
Tupo hewani tena.. kipindi chako pendwa cha STAA WA WIKI ⚽ 🔥
Katika siku ya Leo nakuletea Mchezaji Bora wa wiki hii kutoka kisiwa kidogo kabsaa barani Afrika cha Comoros...
Staa huyu ni Chaker Alhadhur (30), Mlinzi wa kushoto wa klabu ya AC Ajaccio ya Ufaransa na timu ya taifa ya Comoros.
Ipo hivi bhana, Jana Kwenye mashindano ya Kombe la Mataifa AFCON21 dhidi ya Cameroon mlinzi huyu alicheza kama Golikipa baada ya makipa wote 3 wa timu yake ya taifa Comoros kukutwa na korona.
Takwimu zake kwenye mechi hiyo hizi hapa.
Mipira aliyogusa - 52
Pasi alizopiga - 42
Saves alizofanya - 4
Clearance - 1
Karuhusu mabao - 2 tu!🔥
Kutokana na mechi ilivyokuwa ngumu baada ya Mlinzi wa kati na nahodha wao wa Comoros kupewa kadi nyekundu, bado Golikipa huyu alionesha uwezo mkubwa sana, licha ya mashambulizi yote bado aliruhusu mabao machache tu (2). Nayo kitalaamu, yani kutokana na mazoea ya kuwa Mlinzi akupaswa kufungwa, maana alikuwa anajisahau na kuficha mikono nyuma akiogopa kushika, akisahau kuwa yeye ndio Golikipa, kwaiyo kushika na kudaka ndio kazi yake.
Chaker Alhadhur ameonesha ubora mkubwa sana.
Lakini tusisahau umoja na jitihada za timu nzima. Comoros imeingia kwa mara ya kwanza hatua ya 16 ya mtoano katika Kombe la Mataifa AFCON na wamefanya maajabu yafuatayo
☑️ Mara yao ya kwanza kushiriki AFCON
☑️ Wameingia hatua ya 16 bora baada ya kuwafunga Ghana 🇬🇭
☑️ Beki wao wa kushoto amecheza nafasi ya Golikipa na kucheza kwa kiwango kikubwa
☑️ Wamepata kadi nyekundu dakika ya 7 lakini wamefanikiwa kupata goli mbele ya Cameroon 🇨🇲
Hawa ni mashujaa Comoros 🇰🇲 What a team!
Kwa mechi ya jana dhidi ya Cameroon, wadau wa SOKA wanasema kuwa "Cameroon walishinda mechi, lakini Comoros walishinda mioyo yao ❤️"
Post a Comment