RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI MBALIMBALI, PROF. ULINGETA ATEULIWA UENYEKITI TANTRADE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi wafuatao:-

1. Amemteua Prof. Ulingeta Mbamba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TANTRADE).

Prof. Mbamba anachukua nafasi ya Dkt. Ng'wanza Kamata Soko aliyemaliza muda wake.

Prof. Mbamba ni Profesa Mshiriki na Amidi wa Shule Kuu ya Biashara, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

2. Amemteua Bi. Zuhura Sinare Muro kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).

Bi. Muro ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ushauri Elekezi ya Kazi Service Limited na Mkufunzi wa muda katika Taasisi ya Uongozi
(Uongozi Institute), Dar es Salaam.

3. Amemteua Prof. Leonard James Mselle kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya TEHAMA.

Prof. Mselle ni Mhadhiri, Rasi Ndaki ya Sayansi za Kompyuta na Elimu Angavu, Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

No comments