𝐒𝐈𝐌𝐁𝐀 𝐘𝐀𝐖𝐀𝐓𝐀𝐇𝐀𝐃𝐇𝐀𝐑𝐈𝐒𝐇𝐀 𝐖𝐀𝐒𝐈𝐎𝐉𝐔𝐀 𝐖𝐀𝐉𝐈𝐁𝐔 𝐖𝐀𝐎


➪Uongozi wa klabu ya Simba umefanya kikao na benchi la ufundi na wachezaji wakiwataka baadhi yao kutambua thamani na ukubwa klabu ya Simba

➪Mabosi wa Simba walilazimika kukutana na wachezaji na benchi la ufundi kufanya kikao baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Kagera Sugar

➪Ulikuwa ni mchezo wa tatu Simba imeshindwa kupata ushindi ikipoteza mechi mbili na sare moja

➪Katika kikao hicho ambacho kiliwahusisha viongozi wote waandamizi, kilikuwa maalum kujadili mfululizo wa matokeo mabaya na kukumbushana uwajibikaji hasa kwa wachezaji

➪Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again' amesema si jambo la kawaida kwa Simba kupata matokeo kama haya mfululuzo, inaumiza lakini ni wakati wa kutulia na kuangalia nini cha kufanya

➪Try Again amesema hawana tatizo na benchi la ufundi chini ya kocha Pablo Franco kwani timu ilikuwa ikifanya vizuri kabla hadi kutwaa kombe la Mapinduzi. Hata hivyo amesema hawatasita kuchukua hatua pale watakapoona inafaa

➪"Kocha amechukua ubingwa wa Mapinduzi, amefanya vizuri kwenye mechi nyingi tangu alipojiunga na Simba, sioni tatizo la kocha. Japo nasisitiza si jambo la kawaida kwa Simba kupoteza mechi mfululizo, inaumiza"

➪"Kama klabu tutafanya uamuzi sahihi kwa wakati sahihi, mashabiki na wapenzi wa Simba watulie Simba ina viongozi makini na tutapata majibu sahihi kwenye hili," alisema Try Again


No comments