AMKA NA BWANA LEO 16/01/2022
Ndipo akaletewa watoto wadogo ili aweke mikono Yake juu yao na kuwaombea; wanafunzi wake wakawakemea. Mathayo 19:13
▶️ Katika siku za Yesu kina mama walileta watoto wao kwake, ili kwamba aweke mikono Yake juu yao akiwabariki. Kwa tendo hili walionesha imani yao kwa Yesu na shauku kuu ya mioyo yao kwa mafanikio ya sasa na ya baadaye ya watoto hawa waliopewa kuwatunza. Lakini wanafunzi hawakuona uhitaji wa kumkatisha Mwalimu kwa ajili tu ya kuwatambua watoto, na wakati wakiwafukuza kina mama hawa waondoke Yesu aliwakemea wanafunzi na aliamuru makutano kuwapisha njia kina mama hawa waaminifu na watoto wao wadogo. Alisema Yesu, "Waacheni watoto wadogo waje kwangu; wala msiwazuie; kwa maana walio mfano wa hao, ufalme wa mbinguni ni wao."
▶️ Wakati akina mama wakipita katika barabara ya vumbi na kukaribia karibu na Mwokozi, aliona machozi yaliyotiririka bila kutarajiwa na mdomo uliotetemeka, walipokuwa wakiomba kimya kimya kwa niaba ya watoto. Alisikia maneno ya kukemea kutoka kwa wanafunzi, na mara moja akatangua agizo lao. Moyo Wake mkuu wa upendo ulifunguliwa ili kuwapokea watoto. Aliwachukua mmoja hadi mwingine mikononi Mwake na kuwabariki, wakati mtoto mmoja mdogo akiwa amelala usingizi mzito, ameegemea kifuani Mwake. Yesu alinena maneno ya kutia moyo kwa kina mama hawa kuhusu kazi yao, na lo, faraja ya pekee kiasi gani ililetwa akilini mwao! Je, walijawa na furaha kiasi gani walipokuwa wakiutafakari wema na rehema ya Yesu, wakati walipokumbuka tukio hilo la kukumbukwa! Maneno Yake mazuri yaliondoa mzigo kutoka mioyoni mwao na kuwatia moyo kwa tumaini na ujasiri mpya. Hisia zote za uchovu zikatoweka.
🔘 Hili ni somo la kutia moyo kwa akina mama kwa wakati wote. Baada ya kufanya kwa ubora kadiri wawezavyo kwa ajili ya faida ya watoto wao, wanaweza kuwaleta kwa Yesu. Hata watoto wachanga wakiwa mikononi mwa mama zao ni wa thamani sana machoni Pake. Na wakati moyo wa mama ukihitaji sana msaada anaojua hawezi kuutoa, neema ambayo hawezi kuitoa na hivyo kujiweka mwenyewe na watoto katika mikono ya rehema ya Kristo, Yeye atawapokea na kuwabariki, atawapatia mama na watoto amani, matumaini, na furaha.
MWENYEZI MUNGU AKUBARIKI SANA
Post a Comment