AMKA NA BWANA LEO 14/01/2022

*KESHA LA ASUBUHI* 

  *IJUMAA, JANUARI 14, 2022* 

 *OMBA KWA AJILI YA HEKIMA NA NGUVU* 

" _Kama ayala aioneavyo shauku mito ya maji. Vivyo hivyo nafsi yangu inakuonea shauku, Ee Mungu. Nafsi yangu inamwonea kiu MUNGU, Mungu aliye hai_ ." Zaburi 42:1, 2.

▶️ Wale ambao wakati wa Pentekoste walivikwa nguvu kutoka juu hawakuwa wamewekwa huru dhidi ya majaribu na mitihani. Wakati walipokuwa wakiishuhudia kweli na haki walikuwa wakishambuliwa mara kwa mara na adui wa ukweli wote, ambaye alidhamiria kuwakwapua uzoefu wa Ukristo wao. Walibidishwa kujitahidi kwa nguvu zao zote walizopewa na Mungu kufikia kipimo cha kimo cha wanaume na wanawake katika Kristo Yesu. Kila siku waliombea mgawo mpya wa neema, ili kwamba waweze kupanda juu na juu zaidi kuuelekea ukamilifu.

▶️ Chini ya utendaji wa Roho Mtakatifu hata wale wadhaifu sana, kwa kufanyia mazoezi imani kwa Mungu, walijifunza kuimarisha nguvu zao walizopewa na kuwa wametakaswa, kusafishwa na kuadilishwa. Kwa unyenyekevu walijisalimisha kwa mvuto ubadilishao wa Roho Mtakatifu, walipokea utimilifu wa Uungu na wakaumbwa kwa mfano wa Mungu.

▶️ Kupita kwa muda hakujaleta mabadiliko katika ahadi ya wakati wa kuondoka kwa Kristo ya kumtuma Roho Mtakatifu kama mwakilishi Wake. Kutokutiririka kwa neema ya Mungu kwa binadamu hakutokani na kizuizi chochote kitokacho kwake. Ikiwa utimilifu wa ahadi hauonekani kama vile ulivyopaswa kuwa, ni kwa sababu ahadi hiyo haijathaminiwa inavyostahili. Kama wote wangekuwa tayari, wote wangeweza kujazwa na Roho. Mahali popote uhitaji wa Roho Mtakatifu unapokuwa si jambo la kufikiriwa sana, kumekuwa na ukame wa kiroho, giza la kiroho, uharibifu wa kiroho na kifo. Wakati wowote mambo madogo yanapopewa nafasi, nguvu ya Mungu ambayo ni ya muhimu katika ukuaji na mafanikio ya Kanisa, na ambayo ingeweza kuleta baraka nyingine zote kwenye mtiririko wake, inakosekana, ingawa hutolewa kwa wingi usio na kipimo....

🔘 Makundi ya watendakazi wa Kikristo yanapaswa kukusanyika kuomba msaada maalumu, kwa hekima ya mbinguni, ili waweze kujua namna ya kupanga na kufanya kwa busara. Hasa wangepaswa kuomba kwamba Mungu awabatize mabalozi wateule Wake walioko katika maeneo ya utume kwa kipimo cha wingi wa Roho Wake. Uwepo wa Roho pamoja na wafayakazi wa Mungu kutatoa nguvu ya utangazaji wa kweli ambao sio heshima au utukufu wote ulimwengu ungeweza kutoa.

No comments