AMKA NA BWANA LEO 12/01/2022
*OMBA ILI KUAKISI UPENDO WA KRISTO USIO NA KIPIMO*
*Yeye asiyemwachilia Mwana Wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye?* *Warumi 8:32*
*Je! Ninani awezaye kuupima upendo wa Kristo aliouhisi kwa ajili ya ulimwengu uliopotea wakati akiangikwa msalabani, akipata mateso kwa ajili ya dhambi za wakosaji?* Upendo huu ulikuwa haupimiki, usio na kikomo. Kristo ameonesha kwamba Upendo Wake ulikuwa imara kuliko mauti. *Alikuwa akiukamilisha wokovu wa mwanadamu; na japokuwa alikuwa na pambano la kutisha sana dhidi ya nguvu za giza, bado, katikati ya hayo yote, upendo wake ulizidi kuwa imara na imara zaidi.* Thamani ililipwa ili kununua wokovu wa wanaume na wanawake, wakati, katika mapambano ya nafsi ya mwisho, maneno ya baraka yalitamkwa ambayo yalionekana kusikika kupitia uumbaji: "Imekwisha.".
*Urefu, upana, kimo, kina, wa upendo huo wa kushangaza hatuwezi kuupima. *Tafakari ya kina kisichoweza kulinganishwa cha upendo wa Mwokozi inapaswa kujaza akili, kugusa na kuiyeyusha nafsi, kuboresha na kuinua mapenzi, na kubadilisha kabisa tabia yote.*
Wengine wana maoni machache juu ya upatanisho. Wanafikiri kuwa Kristo aliteseka tu kwa ajili ya sehemu ndogo tu ya adhabu ya sheria ya Mungu; wanadhani kuwa, wakati hasira ya Mungu ilihisiwa na Mwanawe mpendwa, alikuwa na uthibitisho wa upendo na ukubali wa Baba Yake, wakati wote wa maumivu yake makali; kiasi kwamba malango ya kaburi yaliyokuwa mbele Yake yaliangaziwa na tumaini zuri, kuwa alikuwa na ushahidi wa kudumu wa utukufu wake wa baadaye. Hili ni kosa kubwa. Maumivu makali ya Kristo yalikuwa hisia ya hasira ya Baba yake. Uchungu wake wa akili kwa sababu hili ulikuwa mkali sana kiasi kwamba wengi wanaweza kuwa na dhana hafifu juu ya hili.
*Huu ni upendo ambao hakuna lugha inayoweza kuuelezea vizuri. Unapita ufahamu wote. Ni siri kubwa ya utauwa. Nafsi zetu zinapaswa kuhuishwa, kuadilishwa, na kuburudishwa na upendo wa Baba na Mwana kwa mwanadamu. Wafuasi wa Kristo hapa wanapaswa kujifunza kuakisi kwa namna fulani upendo huo wa ajabu kwa matayarisho ya kuungana na wote waliokombolewa katika kutoa "baraka, na heshima, na utukufu, na uweza, una Yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na Yeye Mwana Kondoo, hata milele na milele."*
*MUNGU ATUBARIKI TUNAPOTAFAKARI NENO LAKE*
Post a Comment