AMKA NA BWANA LEO 07/01/2022
IJUMAA, JANUARI 7 2022
KUOMBA KATIKA JINA LA YESU
Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki. 1 Yohana 2:1.
📖 Tunaye mwombezi katika kiti cha enzi cha Mungu, ambaye amezungukwa na upinde wa ahadi, nasi tunaalikwa kuwasilisha maombi yetu mbele za Baba katika jina la Kristo. Yesu anasema: Mkiomba lolote kwa jina Langu, mtapatiwa. Katika kuliwasilisha jina Langu, mnatoa ushuhuda kuwa ninyi mmekuwa wangu, kwamba ninyi ni wana na mabinti zangu, na Baba atawachukulia kama Wake, na kuwapenda kama anavyonipenda Mimi.
📖 Imani yako Kwangu itakuongoza kufanyia mazoezi kwa karibu upendo, kama ulivyo upendo wa mtoto kwa wazazi, vivyo upendo wenu kwa ajili Yangu na Baba. Mimi ni kiungo cha thamani ambacho kwacho moyo na nafsi yako vinafungwa kwa upendo na utii kwa Baba Yangu. Mwoneshe Ba Yangu ukweli kwamba jina Langu ni thamani sana kwako, kwamba unaniheshimu na Kunipenda, na kisha unaweza kuomba kile ukitakacho. Atakusamehe makosa yako, na kukuasili katika familia Yake ya kifalme na kukufanya uwe mwana wa Mungu, mrithi wa pamoja na Mwanawe wa pekee.
📖 Kwa njia ya imani katika jina Langu Atakupatia utakaso na utakatifu ambao utakufanya ufae kwa kazi Yake katika ulimwengu wa dhambi, na kukufanya ufae kwa ajili ya urithi wa milele katika ufalme Wake. Baba amekwishafungua, sio mbingu yote tu, lakini pia moyo Wake wote, kwa wale ambao wanaidhihirisha imani katika kafara ya Kristo, na ambao kwa njia ya imani katika kumpenda Mungu wanarejesha uaminifu wao. Wale wanaomwamini Kristo kama mbeba-dhambi, upatanisho wa dhambi zao, mwombezi kwa niaba yao, kwa kupitia utajiri wa neema ya Mungu waweze kudai hazina za mbinguni....
🔘 Maombi ya moyo wa toba hufungua ghala la hazina za mahitaji, na kutupatia nguvu zake Yeye Mwenye uweza wote. Aina hii ya maombi inamwezesha mwombaji kuelewa kile inachomaanisha kupokea nguvu ya Mungu, na kufanya amani na Yeye. Aina hii ya maombi inatuwezesha kuwa na mvuto kwa wale ambao tunahusiana nao.... Ni fursa na jukumu letu kuleta ufanisi wa jina la Kristo katika maombi yetu, na kutumia hoja zile zile ambazo Kristo ametumia kwa niaba yetu. Kisha maombi yetu yatakuwa katika upatanifu kamili na mapenzi ya Mungu.
MWENYEZI MUNGU AKUBARIKI SANA
Post a Comment