AMKA NA BWANA LEO 19/12/2021
*CHAGUENI HIVI LEO*
*Chagueni hivi leo mtakayemtumikia.* *Yoshua 24:15*
Upepo unaongezeka kiasi kwamba unaleta dhoruba. Wala siendelei kuwa juu ya uwanda wa meli [on the steamer Wairarata]. Ninajisikia furaha kutulia.
*Nilikuwa nikiuinua moyo wangu kwa Mungu kwa ajili ya Kristo, ambaye aliutuliza upepo mkali, kusema "Amani, tulia.” Upinde wa mvua wote mara moja ukaenea mbinguni. Nikaiona ishara ya ahadi ya Mungu katika upinde kwenye mawingu, na nikajazwa na ujasiri kwa mikono ya ulinzi wake.*
Mwanamke aliyekuwa akisubiri [n.k., muuguzi wa uwakili] alikuwa mwema kwangu. Nikampatia Hatua za Ushindi Maishani na baadhi ya karatasi na vitini. Nilizungumza naye kuhusiana na wokovu wa roho yake. Nikamwonesha hatari ya kila mmoja ambaye uhai wake ulikuwa baharini. Akasema amelifikiria hili mara nyingi, lakini akasema, "Kama ningeweza, ningekuwa Mkristo, lakini siwezi. Itakuwa vigumu kumtumikia Mungu katika chombo kama hiki. Huwezi kujua, huwezi kuwa na uelewa wa ubaya wa mabaharia hawa. Nahodha na wenza wake wanakaribiana sana katika tabia sawa sawa na kundi la mabaharia kiasi kwamba hawana ushawishi wa kuanzisha matengenezo, kama wakihitaji kitu hicho." Nilimwuliza kwa nini asitafute ajira nyingine. Akasema, "Haitasaidia. Ninao watoto wanne wa kuwasaidia na sina nguvu za kuweza kufanya kazi ngumu." Alikuwa ni mwanamke mdogo, maridadi, aliyekuwa na mwonekano mzuri.
*Nilijaribu kumfafanulia hatari ya kuishi maisha yasiyo ya maombi. Alisema, "Sio kazi yetu kuomba hapa, au kujaribu kuwa watu wa kidini." Nilimwambia kama Bwana amemchagulia sehemu ile ataweza, kama akimpokea Kristo kama Mwokozi wake, na kumkubali Kristo kama kimbilio lake. Alijibu, akiwa na machozi machoni pake, kuishi maisha ya dini hapa. Natumaini siku moja nitapata sehemu "Haiwezekani. Nawafahamu marafiki nilionao kwenye meli hii. Siwezi wazi kwangu ambapo nitaweza kuisaidia familia yangu, na ndipo nitakapokuwa makini kwa mambo muhimu. Laiti kama ningekuwa na watoto wangu na kuwasaidia kwa njia rahisi ningefurahia kuchagua kufanya hivyo."*
*MUNGU ATUBARIKI TUNAPOTAFAKARI NENO LAKE*
Post a Comment