AMKA NA BWANA LEO 08/12/2021
*UKAIDI — KIZUIZI KWA MAENDELEO YOTE.*
*Nilijua ya kuwa wewe u mkaidi, na shingo yako ni shingo ya chuma, na kipaji cha uso wako ni shaba. Isaya 48:4.*
▶️ Ukaidi ni aina mbaya ya tabia, na kama isipokomeshwa, inakuwa ni njia ya kufanya mabaya mengi. Yeye ambaye ni mkaidi hatatoa maoni yoyote ambayo anaweza kuwa nayo. Upungufu wa akili ni kisababishi cha ukaidi. Kuna watu wenye uwezo wa kiakili ambao wameruhusu ukaidi kukua katika tabia zao, na wanakataa kuamini mambo ambayo ni sahihi, kwa sababu tu wao wenyewe hawakuyaanzisha.
▶️ Ukaidi ni kikwazo kwa maendeleo yote. Mtu mkaidi hataweza kushawishiwa na jambo lolote ambalo akili yake haiwezi kulielewa. Hajui inamaanisha nini kutembea kwa imani. Huzingatia tu mipango na maoni yake mwenyewe, yakiwa sahihi au mabaya, kwa sababu amekwisha asili aina hii ya mawazo. Anaweza kuwa na sababu za kutosha kuona kuwa amekosea; ndugu zake wanaweza kuzungumza kinyume na maoni yake, na mbinu zake za kuweza kufanikiwa katika kazi, lakini anathamini msimamo wake dhidi ya usadikisho.... Atapendekeza maoni ambayo hayakubaliki kwa uzoefu au kwa maamuzi ya watu ambao wana akili timamu na wenye hekima kama yeye alivyo. Atatoa madai kana kwamba alikuwa akijua yote yanayokuja, na atashikilia maoni yake kuwa ya kutosha. Ubinafsi umekuwa kwa muda mrefu sehemu ya kumtawala, kiasi kwamba kwa bahati mbaya mtu huyu anaona kuwa ni fadhila kama anavyofikiri, kuwa na akili kama aliyo nayo. Kama njia yake haikufuatwa, ataibua vipingamizi kwa kila tukio, katika mambo madogo na makubwa. Atayashikilia maneno yake, yakiwa ni ya kweli, au uongo kabisa. Mazoea haya, yanaporudiwa mara kwa mara, yanathibitika kuwa mambo yasiyopendeza, na yanakuwa tabia.
▶️ Na wawili au watatu ambao wamefanya ukosoaji kuwa sayansi yao, wanaochukua nafasi katika upinzani kwa takribani kila kitu, wanaweza kuishusha chini biashara iliyo bora kabisa. Wanaweza kuotesha mbegu za mashaka kuliko wanavyoweza kutamani kuona zikiiva mpaka kuvunwa....
▶️ *Bwana hafurahii kuona roho hii ikizuia na kuharibu kazi yake. Anawaita watu watakaotimiza mapenzi yake, watu watakaotawaliwa na Roho Wake Mtakatifu.*
*MUNGU ATUBARIKI SOTE.*
Post a Comment