AMKA NA BWANA LEO 07/112/2021
*HASARA YA MILELE*
_Jicho halikuyaona, wala sikio halikuyasikia, (wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,) mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao. 1 Wakorintho 2:9._
📖 Kila dhambi, kila tendo lisilo la haki, kila uasi wa sheria ya Mungu, husema kwa nguvu mara elfu zaidi kwa mtendaji kuliko kwa mtendewa. Kila wakati moja ya fani tukufu ambazo Mungu amemkabidhi mwanadamu isipothaminiwa na kutumiwa vibaya, fani hiyo hupoteza milele sehemu ya nguvu yake na haiwezi kuwa kama vile ilivyokuwa hapo kabla ya unyanyasaji huo. Kila dhuluma ifanywayo dhidi ya asili ya utu wetu katika maisha haya hutuathiri sio kwa muda tu bali hata milele. Japo Mungu anaweza kumsamehe mdhambi, lakini umilele hautarudisha upotevu huo wa hiari ulioendekezwa katika maisha haya.
📖 Ili kuendelea katika hatua ifuatayo, ya maisha ya baadaye, huku ukiwa umenyimwa nusu ya nguvu ulizopaswa kuwa nazo kuwa pale ni wazo linaloumiza sana. Wakati wa rehema uliopotezwa hapa katika kupata utayari wa mbinguni, ni hasara ambayo haiwezi kufidiwa. Uwezekano wa kustarehe utakuwa mfinyu sana katika maisha ya baadaye kwa wakosaji na kwa matumizi mabaya ya nguvu za maadili katika maisha haya. Haidhuru ni kiasi kikubwa jinsi gani tunaweza kupata katika maisha, tunaweza kupaa juu na hata juu zaidi kama tungetumia zaidi fadhila tuliyopewa na Mungu na fursa za dhahabu za kuboresha uwezo tuliopewa hapa katika uwepo wa rehema....
📖 Sisi sote tupo chini ya mmoja au mwingine kati ya manahodha wakuu wawili. Mmoja, Mwumbaji wa mwanadamu na wa dunia, ni mkuu wa wote. Wote wanatakiwa kumpa utii wao mkamilifu, kumpa upendo wao wote. Ikiwa akili imewekwa katika utawala Wake, na kama Mungu ndiye mtengenezaji na mwendelezaji wa nguvu za akili, nguvu mpya za maadili zitakuwa zikipokelewa kila siku kutoka kwa chanzo cha hekima yote na nguvu zote. Baraka za maadili na uzuri wa Uungu zitatoa thawabu kwa juhudi za kila mtu ambaye akili yake imeinamia mbinguni. Tunaweza kuuelewa ufunuo-uzuri wa mbinguni, ambao uko mbali zaidi ya maono mafupi ya ulimwengu, ambao unazidi mawazo ya akili kubwa zaidi ya mwanafalsafa aliyesoma sana ambaye hajajiunganisha na nguvu ya milele....
🔘 *Haki, heshima, upendo na ukweli ni sifa za kiti cha enzi cha Mungu. Hizi ni kanuni za serikali yake ambayo inapaswa kuanzishwa hapa duniani, zilizosafishwa kwa moto wa malipo ya haki yake. Hivi ni vito vya thamani kutafutwa na kutunzwa kwa muda na kwa umilele. Kwa mtazamo wa mambo hayo, ... jenga tabia yako sio kwa viwango vya ulimwengu, bali kwa vya mbinguni.*
MUNGU AKUBARIKI SANA
Post a Comment