UMESHAWAHI KUJIULIZA.? KLABU YA NEWCASTLE UNITED NA MAPINDUZI YA SOKA JE? WATAWEZA KWELI?
Klabu ya Newcastle United na mapinduzi ya Soka Je wataweza kweli? Nakumbuka mnamo mwaka 2003 kuelekea 2004 kwenye Ligi Kuu ya Uingereza kulifanyika mapinduzi makubwa kisoka na mapinduzi yenyewe sio mengine bali ni uwekezaji wa Bilionea Roman Abromovic pale ndani ya Klabu ya Chelsea.
Bilionea yule akapiga hodi pale akaitikiwa na akapewa baraka zote za kuimiliki Klabu ya Chelsea, kitu cha kwanza huyu jamaa akapanga mifumo yake haswa kwenye maswala ya kiutawala na benchi la ufundi kwa kumleta kocha Jose Morinho kutoka Klabu FC Porto ya Ureno na kumleta aliyekuwa mtendaji mkuu wa Manchester United Peter Kenyon ili aje kuwa mtendaji mkuu pale Chelsea FC..
Kweli zoezi ilo likafanikiwa watu hao wakaungana na kutengeneza Chelsea iliyokua bora na sio Uingereza tu bali mpaka Ulaya kwa ujumla ulikua ukitaka kupata matokeo kwa Chelsea ata ayo ya sale tu ujipange kwelikweli.
Chelsea ikazidi kufanya vizuri katika msimu uleule wa kwanza wa ujio wa Bilionea abromovic na hatimae mwisho wa msimu wakawa mabingwa wa taji la Ligi Kuu ya Uingereza.
Kuanzia hapo mpaka sasa Klabu ya Chelsea FC ikafanikiwa kukusanya idadi kubwa ya mashabiki karibu kila engo ya dunia hii kadri miaka ilivyozidi kwenda mbele Chelsea ikazidi kutwaa Mataji ikiwemo taji labUEFA CHAMPIONS LEAGUE.
Oky, Tunaamia kwenye Ywekezaji wa Klabu ya Newcastle United na hadisi zao za kusadikika je wataweza kweli? Shughuli yake pevu na sio ya kipolepole ata kidogo kwanza kabisa inaitaji uwe na fungu la kutosha pili uwe na utawala shupavu shupavu usioyumbayumba na ndio apo kinapokuja kitu cha tatu ambacho sio kingine bali ni kufurahia matokeo ya kile mlichokiwekeza vinginevyo watakuja kuludia yaleyale ambayo wamepitia timu kama Tottenham hotspur, Leicester City kwa kuonja radha ya kushiriki mashindano ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE.
Lakini kwa sasa nafasi iyo hawaipati tena na yote kwa sababu gani kipindi wakati wanapata nafasi izo timu kubwa zilishuka sana kiwango.
Lakini kwa sasa wafalme wa Ligi ya Uingereza wameludi kwenye ubora ndio mana unaona hao kina Leicester City, Tottenham Hotspur, hawatambi tena.
Kwa hiyo nimmegee siri moja uyu mzee wangu Bilionea wa kisaudia aliokuja kuwekeza katika Klabu ya Newcastle United inatakiwa wakati anajiandaa kumleta kocha pamoja na wachezaji wenye ubora lazima pia akumbuke kutengeneza shepu bora ya kiutawala kwani utawala bora na ulio imara ndio kila kitu katika taasisi yoyote ile duniani inayotaka mafanikio makubwa.
Imeandikwa Na Mwanahabari Wa Binago Kutoka Morogoro Mr. Pembe Seleman Machupa..!✍.
Post a Comment