MUNGU NI PENDO
*Mungu ni PENDO*
Yohana:3.16
“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.”
Yohana:3.17
“Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. ”
Hakika Mungu ni pendo, na dhana halisi ya upendo wake tunauona pale alipo upenda ulimwengu/walimwengu walipokuwa wangali katika dhambi.
Hakika hili ni pendo kuu mno maana tulipokuwa katika hali ya dhambi, yeye aliamua kumtoa mwanae wa pekee asiyekua na dhambi kabisa/mtakatifu na mwenye haki ili aichukue dhambi yetu, afanyike mdhambi kwa kuibeba dhambi yetu, apokee mshahara wa dhambi (mauti) kwa niaba yetu KISHA mwisho wa siku afufuke na kwa kufufuka huko iwe ni ishara ya kuishinda dhambi. (ondoleo la dhambi)
Kwa kule kufanyika kwake mdhambi bila kutenda dhambi yeyote ile, Hivyo sisi nasi tufanyike watakatifu kwa kutokutenda jambo lolote lile.
Ondoleo la dhambi kwetu wanaadamu ni ZAWADI, ni kitu tunachopaswa KUKIAMINI na kukipokea kwa mikono miwili bila kuulizauliza maswali.
Ni jambo ambalo sisi kwa juhudi zetu binafsi tulishindwa kulifanya.
Mungu kwa rehema zake na pendo lake lililo kuu kupita fahamu zetu, aliamua kutupa zawadi. Kwa kupitia mwanae mpendwa Yesu Kristo tumeipokea zawadi hio.
Ni kiburi tu kuona kama sisi tunauwezo binafsi wa kuikimbia dhambi, ila ni jambo la busara na hekima sana kusema asante Mungu kwa kututua mzigo wa dhambi uliokua ukituelemea vichwani mwetu, kwa kupitia mwanao mpendwa Yesu Kristo.
Yohana 3:16 Inatudhihirishia wazi kua Mungu alitupenda tungali wenye dhambi hivyo akamtoa mwanae wa pekee ili kila amwaminie asipotee bali awe na uzima wa milele.
Kumbe tunaona dhahiri kuwa tulipokuwa katika hali ya dhambi tulikua upotevuni, na hivyo kwa kutolewa kwa sadaka ya Yesu Kristo tumepata karama ya *UZIMA WA MILELE.*
Neno UZIMA WA MILELE linamaanisha MILELE kweli kweli, yaani ni Uzima usio na mwisho, usio chacha wala ku expire, ni wa milele tangu pale mtu alipo upata mpaka milele yote.
Uzima huu wa milele hauwezi kupotea kamwe kwa yeyote yule aliye upokea, ni wa milele hivyo hivyo kama ulivyoitwa wa milele.
Yohana:10.28
“Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu.”
Yohana:10.29
“Baba yangu aliyenipa hao ni mkuu kuliko wote; wala hakuna mtu awezaye kuwapokonya katika mkono wa Baba yangu. ”
Asiye nao uzima huo wa milele yuko upotevuni milele, Ila wewe UAMINIYE kuwa Kristo Yesu alikufa kwa ajili ya ondoleo la dhambi yako basi unao uzima wa Milele na hauta potea kamwe kwa namna iwayo yoyote ile.
Yohana 3:17 inasema kwa maana Mungu hakumtuma Yesu auhukumu ulimwengu bali ulimwengu uokolewe katika yeye.
Kumbe tunaona dhahiri kuwa kusudio la Mungu hata tulipokua wenye dhambi halikua kutuhukumu bali kutuokoa. Hakika hili ni pendo la ajabu sana atuonyeshalo yeye kama Baba yetu, aliona tatizo na hakutaka kutuhukumu kwa hilo bali kutuokoa kwa kututoa kutoka kwenye dhambi hiyo na kutufanya watakatifu wake na kutupa uzima wa milele.
Yohana 3:18
“Anasema amwaminie yeye hahukumiwi, asieamini amekwisha kuhukumiwa kwakuwa hakuliamini jina la mwana pekee wa Mungu.”
Alaaah!! Kumbe tunaona dhahiri kuwa kwa kuamini kwetu juu ya ondoleo la dhambi kupitia Kristo Yesu basi tunakuwa tumeokolewa tayari na hatuhukumiwi, ila kwa kuto kuamini kwetu basi ndio kujiweka hukumuni, yaani Ukiamini hauhukumiwi milele, na usisipo amini unahukumiwa, kwasababu tu hujaamini ondoleo la dhambi kupitia Yesu hivyo inamaana dhambi kwako bado ipo hivyo utahukumiwa kwa kuto kuamini kwako.
Hivyo napenda kulielezea pendo hili la Mungu kwako leo kuwa Mungu anachotaka tu ni wewe uamini kuwa Kristo alikufa kwa ajili yako, aliibeba dhambi yako, akafa kwa niaba yako, akafufuka kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako.
Ujue kuwa ukisha muamini Kristo, basi yeye anakaa ndani yako nawe unakaa ndani yake
1 Yohana:4.14
“Na sisi tumeona na kushuhudia ya kuwa Baba amemtuma Mwana kuwa Mwokozi wa ulimwengu. ”
1 Yohana:4.15
“Kila akiriye ya kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu, Mungu hukaa ndani yake, naye ndani ya Mungu. ”
Na ufahamu kuwa ukishakuwa ndani ya Kristo basi kamwe hauna hukumu ya adhabu mbele yako milele na milele
👇
Warumi:8.1
“Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu. ”
Ulibadilishana na Kristo wewe ukampa dhambi zako yeye akakupa utakatifu wake, Akaishinda dhambi.
(Waebrania 12;4
*Hamjafanya vita hata kumwagika damu, mkishindana na dhambi* )
yako hivyo wewe na yeye mu watakatifu, mu wana wa Mungu na mu-wenye haki mbele za Mungu hata milele na yeye, ufahamu kuwa wewe u-mtakatifu wakati huu ungalipo duniani, kama Kristo alivyo hivyo hivyo nawe ndivyo ulivyo ulimwenguni humu.
1 Yohana:4.16
“Nasi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini. Mungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake. ”
1 Yohana:4.17
“Katika hili pendo limekamilishwa kwetu, ili tuwe na ujasiri katika siku ya hukumu; kwa kuwa, kama yeye alivyo, ndivyo tulivyo na sisi ulimwenguni humu. ”
*SASA JE TUTAPATAJE KUPONA TUSIPO UJALI WOKOVU MKUU NAMNA HII.*
Niseme tu kuwa Mungu anakupenda sana na usiache kuwashirikisha na wengine pendo hili la Mungu wetu. Amen
*Umebarikiwa*
*Siku njema/Kazi njema.*
*🌹 🌹*
Post a Comment