MAONO KWA VIJANA

*SOMO* :
 *OMBA MUNGU* *AKUONYESHE* *UTUKUFU WAKO* *UJAO ILI UWEZE* *KUHIMILI* *CHANGAMOTO* *UNAZOZIPITIA LEO* "

 *Warumi 8:18* 
" Kwa maana nayahesabu mateso ya wakati huu wa sasa kuwa si kitu kama utukufu ule utakaofunuliwa kwetu..

Kinachokufanya ukate tamaa sasa na kuvunjika moyo ni kwa sababu hujaiona kesho yako ilivyo bora kuliko Leo

Laiti kama ungeiona kesho yako iliyojaa Baraka furaha na amani *UNGEIDHARAU* *AIBU YA LEO* ...

Ni kweli Leo maskini unanyanyaswa...ni kweli Leo umeachwa na mchumba...ni kweli Leo huna kazi...ni kweli Leo huna mtoto... Ni kweli Leo huna mtaji na kila anayekuona anakudharau..... *SIKIA MTU WA MUNGU NI KWA SABABU HUJAIONA KESHO YAKO NDIYO MAANA UNALIA...*..

Kilichomfanya Yesu avumilie mateso na aibu ya msalaba ni kwa sababu alijua baada ya kushinda kifo/mauti hata kuwa Yesu Wa kawaida " *ATAKIRIMIWA JINA* *LINALOPITA* *MAJINA YOTE* "....

Anza kuiona kesho yako kwanza kabla hujaiona Leo yako iliyo ya machozi na huzuni... *HATA HILO LITAPITA KAMA YALE YALIVYOPITA CHINI YA MSALABA WA YESU*

Mtume Paul anasema .. nayahesabu mateso ya wakati huu kama si kitu kwa sababu ya ule utukufu ujao anaouona.... *UTUKUFU WA KESHO UNAMFANYA ADHARAU MATESO YA SASA HIVI NA KUONA SI KITU!!!...* 

Unajua kuna nyakati unaweza kuzipitia ukadhani utafia hapo ..yaani macho yako yanajaa machozi mpaka huioni kesho yako... Yaani unaweza kudharauliwa mpaka ukajiona ni kiumbe uliyekosea kuzaliwa....

Nataka kukuambia mateso unayopitia kazini kwako/kwenye ndoa/kwenye familia/kwenye Huduma/kwenye masomo/kwenye uchumi/kwenye Nyumba ya kupanga/ 
 *YAONE SI KITU* *KWA SASA MAANA* *BWANA* *ATAENDA* *KUKUINUA KWA* *UTUKUFU MKUBWA* *KIASI* *UTASAHAU* *MATESO YAKO* *YA LEO* ..

HILI NI OMBI LANGU KWA MUNGU AFUNGUE MACHO YAKO UIONE KESHO YAKO,
 KISHA FUTA MACHOZI IDHARAU AIBU YA LEO NA KUONA SI KITU KWA JINSI MUNGU ATAKAVYOKUBARIKI 

"Lakini akiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa kutokuamini, bali alitiwa nguvu kwa imani, akimtukuza Mungu;"

 *Warumi 4:20* 
Mpendwa Yesu Kristo ana makusudi na MAISHA Yako yale unayopitia leo yawe magumu yasikuharibie maono Kumbuka kesho Yako ni kubwa Sana kuliko leo yako
    *JIFUNZE HAPA KUNA JAMBO ZITO LITAKUFUNGUA*
👇👇👇👇👇👇
https://youtu.be/1x-6Gqc5c-o
 *MUNGU MBARIKI MTU ATAKAYE SHARE UJUMBE HUU KATIKA JINA LA YESU KRISTO*

No comments