AMKA NA BWANA LEO 30/11/2021
JUMANNE, NOV 30 2021
*UONGOFU WA KILA SIKU*
_Mizani ya hadaa ni chukizo kwa Bwana; Bali vipimo vilivyo sawasawa humpendeza. Mithali 11:1._
▶️ Tunahitaji kuongoka kila siku. Ikiwa umenufaika katika shughuli zako za biashara, kwa njia ambayo Bwana anaiita dhuluma, jambo hili lazima lirekebishwe ili uwe mwaminifu na mwenye haki mbele za Mungu. Mambo haya lazima yasahihishwe na watu wetu kila mahali.... Unapoanza kazi hii ya kujirekebisha na kujiweka sawa mbele ya Mungu, malaika wa mbinguni watashirikiana nawe, wakikupatia utambuzi wa kuona mahali ambapo mtazamo wako wa mambo una kasoro.
▶️ Kristo na malaika wanaitazama kazi yako. Wanapima kila tendo. Hebu maisha yako yamwakilishe Kristo mnyenyekevu na mpole. Jitahidi kutenda kama ambavyo Kristo angetenda kama angekuwa katika nafasi yako. Kusiwepo tofauti kati ya kipimo chako cha uaminifu na kipimo cha Mungu. Kanuni safi, na za kweli lazima ziongoze maisha ya kila roho ambayo itatangazwa kuwa ya haki na takatifu siku ya Mungu.
▶️ Kuna miamala mingi katika ulimwengu wa kibiashara ambao watu wa ulimwengu huchukulia kuwa ya haki na uaminifu, lakini ambayo Mungu anaikataa. Watu huweka mipango ambayo wanaiona kuwa ni mipango sahihi, lakini ambayo haikubaliani na kanuni za kweli, zisizokuwa za uchoyo ambayo Kristo aliweka katika Neno Lake.... Lakini kibali cha ulimwengu hakiwezi kuyafanya matendo ya udhalimu kuwa ya haki, na kosa litabaki kuwa kosa mbele za Mungu mpaka liungamwe na kuachwa.
▶️ Bwana hawezi kuwabariki watu wanaojinajisi kwa shughuli za kibiashara za udhalimu, ama wakiwa na waumini wenzao au na watu wa ulimwengu. Na watu wanaofanya mambo kama hayo wanapoteza hali yao njema ya kiroho; wanakuwa baridi, wa dini ya mtindo tu na wabinafsi. Wanapamba makosa yao ya zamani kwa nadharia walizozigundua wenyewe zilizo kinyume na kanuni za Neno la Mungu.
▶️ Kanuni inayopaswa kutawala kila shughuli ya kibiashara imeelezwa wazi na Kristo. "Basi yo yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo torati na manabii" (Mathayo 7:12)....
🔘 *Upumbavu, kuwafikiria wengine vibaya, kuinua nafsi, mambo ambayo huharibu juhudi za kweli vitaachwa kabisa, na waumini wa kweli watakuwa wanyenyekevu wa moyo, na watakuwa na bidii katika kazi zao kwa ajili ya roho zinazoangamia.*
*MUNGU AKUBARIKI SANA*
Post a Comment