AMKA NA BWANA LEO 29/11/2021

JUMATATU, NOV 29 2021

*HUDUMA YA MALAIKA WA MBINGUNI*

_Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu? Waebrania 1:14._

📖 Bwana hawaachi gizani wale wanaofuata nuru yote waliyopewa, bali hutuma malaika Wake waongee nao. Kornelio aliishi kulingana na maagizo yaliyotolewa katika Maandiko ya Agano la Kale, na Bwana alimtuma mjumbe ili amwambie yampasayo kufanya.

📖 Mungu angeweza kumpa Kornelio mafundisho yote kwa njia ya malaika, lakini huu haukuwa mpango Wake. Mpango Wake ulikuwa kumwunganisha Kornelio na wale waliokuwa wamepokea nuru kutoka juu, watu ambao kazi yao ilikuwa kugawa nuru hii kwa wale waliokuwa wakiitafuta nuru. Hivyo ndivyo Mungu anavyoshughulika na watu Wake.

📖 "Peleka watu Yafa," malaika alisema, "ukamwite Simoni, aitwaye Petro. Yeye ni mgeni wa mtu mmoja, jina lake Simoni, mtengenezaji wa ngozi, ambaye nyumba yake iko pwani, atakuambia yakupasayo kutenda" (Matendo 10:5, 6). Kornelio alitii maagizo aliyopewa. Alijiunga na kanisa, na akawa mtendakazi makini na mwenye mvuto pamoja na Mungu.

📖 Mfano huu unapaswa kuwa faraja na nguvu kwetu. Hebu wale walio katika utumishi wa Mungu wajifunze vizuri uhusiano uliopo kati ya mbingu na dunia. Vyombo vya mbinguni na duniani vinapaswa kuungana katika kazi kubwa ya kuwasilisha nuru kwa wale walio gizani. Malaika wa mbinguni wanapaswa kuwasilisha mibaraka kwetu, na sisi tena inatupasa kuitoa kwa wanadamu wenzetu.

📖 Angalia sifa zilizotolewa kwa Kornelio: "Sala zako na sadaka zako zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu" (Aya ya 4). Uaminifu wake ulitambuliwa mbinguni. Mungu aliona kuwa alikuwa mtu aliyestahili kuaminiwa na kupewa nuru kubwa zaidi na majukumu makubwa zaidi, kwa sababu alikuwa amezitumia vizuri talanta alizoazimwa. Inatupasa kuchukuliwa uwakili wetu kuwa wajibu wetu mtakatifu. Inatupasa kufanya kazi kwa bidii kulingana na talanta tulizoaminiwa. Tunapofanya hivyo, Mungu atatambua juhudi zetu na uaminifu wetu, na atatupatia uwezo mkubwa zaidi kwa ajili ya huduma.

🔘 *Mungu anafanya kazi kubwa ya kuwaandaa watu Wake ili wazae matunda kwa ajili ya utukufu Wake. Paulo anasema: "Maana sisi tu wafanya kazi pamoja na Mungu; ninyi ni shamba la Mungu, ni jengo la Mungu" (1 Wakorintho 3:9).*
*MUNGU AKUBARIKI SANA*

No comments