AMKA NA BWANA LEO 24/11/2021
JUMATANO, NOV 24 2021
*UAMINIFU KATIKA SHUGHULI ZA BIASHARA*
_Kwa bidii, si walegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana. Warumi 12:11._
📚 Watumishi wa Mungu wanawajibika, kwa namna moja au nyingine, kujihusisha na ulimwengu kwa njia ya miamala ya biashara. lakini inawapasa kununua na kuuza kwa utambuzi kuwa jicho la Mungu liko juu yao. Mizani ya uongo na vipimo vya udanganyifu visitumiwe. kwa kuwa hivi ni machukizo kwa Bwana. Katika kila muamala wa kibiashara Mkristo atakuwa vile anavyotaka ndugu zake wamfikirie kuwa ndivyo alivyo. Njia zake za utendaji zitaongozwa na kanuni za msingi. Hadanganyi, hivyo, hana cha kuficha. Anaweza kukosolewa. anaweza kujaribiwa, lakini uadilifu wake usiopinda utang'aa kama dhahabu safi. Yeye ni baraka kwa wote wanaoshirikiana naye, kwa kuwa neno lake linatumainiwa. Siyo mtu ambaye anajinufaisha kwa kumdhulumu jirani yake. Yeye ni rafiki na mfadhili kwa wote, na wanadamu wenzake wanaamini ushuri wake....
📚 Mtu aliye mwaminifu na mkweli hatajinufaisha kutokana na udhaifu au upungufu wa wengine ili kujaza mfuko wake. Anapokea malipo yaliyo halali na yaliyo sawa na kile anachokiuza. Ikiwa kuna dosari katika vitu anavyoviuza, anakuwa mkweli na muwazi kwa kumwambia ukweli rafiki au jirani yake, hata kama kwa kufanya hivyo ni kinyume na maslahi yake ya kifedha. Katika mambo yote madogo madogo ya maisha kanuni makini za maisha sharti zizingatiwe. Hizi siyo kanuni zinazotawala uliwemgu wetu, kwa kuwa Shetani-mdanganyaji, mwongo, na mnyanyasaji-ndiye kiongozi, na raia wake wanamfuata na wanatekeleza makusudi yake. Lakini Wakristo wanatumika chini ya Kiongozi mwingine, na matendo yao lazima yatendeke ndani ya Mungu, bila kujali faida zote za kibinafsi. Kutenda kinyume cha haki katika shughuli za kibiashara kunaweza kuonekana kuwa jambo dogo kwa mtazamo wa mtu, lakini Mwokozi hakuchukulia hivyo. Maneno Yake kuhusiana na kipengele hiki ni ya wazi na ya moja kwa moja: "Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia" (Luka 16:10)....
🔘 *Katika ulimwengu wa Kikristo leo udanganyifu unatendwa kwa kiwango cha kutisha. Watu wazishikao amri za Mungu wanapaswa kuonesha kuwa wako juu ya mambo haya yote. Matendo ya udanganyifu yanayochafua mahusiano kati ya mtu na wenzake yasitendwe kamwe na ye yote anayedai kuwa muumini wa ukweli wa leo.*
*MUNGU AKUBARIKI SANA*
Post a Comment