WHO YARIPOTI VIFO 719 VYA CORONA NCHINI TANZANIA
Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti vifo 719 kutokana na virusi vya Corona (COVID-19) huku maambukizi yakifikia 25,846 nchini Tanzania.
Mganga Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Dkt Aifelo Sichwale amethibitisha takwimu hizo zilizoainisha taarifa ya mlipuko huo tangu Januari 03, 2020.
Aidha ripoti hiyo imesema hadi Septemba 23, mwaka huu watu 389,807 walipata chanjo nchini Tanzania.
Siku chache zilizopita, Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan aliendelea kutilia mkazo juhudi katika vita dhidi ya Covid-19.
Rais Samia aliwataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo lakini pia akawataka viongozi wa Serikali kuendelea kutoa elimu juu ya umuhimu wa kila raia kupata chanjo.
Post a Comment