“Wanawake wapeni tendo la ndoa waume zenu, acheni visingizio. Mkiwanyima ndiyo maana wengine wanaamua kuanza kuchepuka matokeo yake
Kwa upande mwingine akasema matukio ya ukatili wa kijinsia katika familia nyingi yamekuwa yakisababishwa na tabia za wanandoa kuanza kusaliti wenza wao matokeo yake wanashindwa kupatiana haki ya ndoa hali inayosababisha wanandoa hao kuanza kuchepuka ili kukidhi haja zao za kimwili.
“Wanawake vunjeni ukimya, fungukeni kuhusu akina baba wanaolala na suruali kwani wanawafanyia ukatili wa kingono kwa kuwanyima haki yenu ya ndoa,” amesema Rahabu.
“Mwanaume kwanini ulale na mke wako huku umevaa suruali? ulioa kwa ajili ya nini,huoni kuwa unamnyima haki yake mkeo na kumfanya awaze kuwa unamsaliti kwa kufanya ngono na wanawake wengine nje ya ndoa. Kwanini ulale na suruali wakati mwenzako anataka.
0 Comments