AMKA NA BWANA LEO 29/10/2021

*KESHA LA ASUBUHI* 

 *Ijumaa, Oktoba 29,2021* 

 *WAKRISTO WANAO ONGOZWA NA ROHO*

" _Sheria ya Bwana ni kamilifu,huiburudisha nafsi. Ushuhuda wa Bwana ni amini, humtia mjinga hekima._ "
Zaburi 19:7

▶️ Katika zama hizi za mapambano,wengi wa wale ambao nuru ya maisha ya kujitoa ya Mwokozi inawaangazia,hawataishi kulingana na kanuni za mbinguni. Wanatamani kufanya maonesho tofauti na aliyofanya Kristo.Ili kukabiliana na ushawishi wa watu hawa,inatulazimu kuinua kiwango cha Ukristo, kwa kuwa wengi wametanga mbali na kanuni za kuwa mfano kama Kristo. Ukweli na haki vimepoteza maana zao halisi kwao....

▶️ Wakati Roho Mtakatifu atakapofanyia kazi akili za Wanadamu, kutakuwa na kiwango cha juu zaidi kwa hotuba, kwa huduma na kwa hali ya kiroho katika makanisa yetu kuliko inavyoonekana sasa. Ndipo washiriki wetu watakapoburudishwa kwa maji ya uzima, na watenda kazi, wakifanya kazi chini ya kiongozi mmoja Kristo,Watamdhihirisha Bwana wao kwa maneno, kwa roho, kwa kila namna ya huduma, na watahimizana sana,Kumaliza kazi iliyokuwa inawahusu.

▶️ Kutakuwa na ongezeko lenye afya la umoja na upendo, ambao utabeba ushuhuda kwa ulimwengu kuwa Mungu alimtuma Mwanawe kwa ajili ya ukombozi wetu. Kutakuwa na kupogolewa kwa matawi ya mzabibu, na uzaaji wa matunda mengi. Na matawi ambayo hayazai matunda ya thamani ya Roho- kunena na kutenda kama Kristo- yatakatiliwa mbali kutoka kwenye shina. Ukweli wa uungu utainuliwa,na unavyo angaza kama taa iwakayo, tutaelewa zaidi na kwa ukamilifu.

▶️ Wale wanaoushikilia Ukweli kwa haki wataamka, na kuvaa viatu vya injili.Miguu yao kufungiwa utayari waupatao kwa kwa injili ya Amani, hawataifuata njia ya uongo ambayo kwa kufanya hivyo vilema kugeuzwa kuiacha njia sahihi.

▶️ *Mungu anamtaka kila mtu asimame peke yake,na kufuata maelekezo ya neno. Katika kila hatua wafuasi wa Kristo wanapaswa kuonesha heshima yao kwa kanuni za Kikristo-* *kumpenda sana Mungu, na jirani zao kama nafsi zao; kuonesha mwanga na baraka kwenye njia ya wale ambao wako gizani;* kuwafariji wale ambao wameangushwa chini; kuyafanya matamu maji machungu katika mahali pa kuwapa wasafiri wenzao nyongo wanywe..... *Tunapaswa kuwa na Ukristo safi unaokua. Katika uwanda wa mbinguni tunapaswa kutangazwa kuwa kamili katika Kristo* .

No comments