AMKA NA BWANA LEO 22/10/2021

*KESHA LA ASUBUHI.*

Ijumaa, 22/10/2021.

*USIWE NA SHAKA.*

*Furahini katika Bwana siku zote; tena nasema, furahini. Wafilipi 4:4.*

▶️ Hii ni fursa kwa kila mtu ambaye ana nafasi katika nyanja yoyote ya kazi ya Bwana kujua kwamba amesamehewa dhambi zake, na kufurahi katika uhakika wa kuwa na maisha ya juu katika uwanda wa juu. Tumaini hili ni la thamani kubwa kuliko fedha au dhahabu au mawe ya thamani. Litunze tumaini hili kuwa angavu daima, na tafuta kuwapatia wengine tumaini hili. Katika kufahamu kuwa tabasamu la Mungu li juu yako, moyo wako utajawa na furaha na Amani.

▶️ Sikiliza mwaliko wa neema ya Kristo, "Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu. Kwa maana nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi" (Mathayo 11:28-30).

▶️ Hebu wote na walitafute lile pumziko ambalo Kristo alituahidi. Unapaswa kuuonesha kwa ulimwengu ukweli wa neno Lake. Unapaswa kuonyesha kwamba katika kujitia nira ya Kristo, kuna furaha ya kweli.

▶️ Usimkosee Mungu heshima kwa kutilia shaka maneno yake. Jinsi unavyomwamini, ndivyo atakavyoshirikiana nawe katika juhudi zako, na katika umoja na yeye, nawe utaweza kufanya kazi inayokubalika. Kupitia kwa haki anayotupatia, mweze kuepuka uharibifu uliopo duniani kwa sababu ya tamaa.

▶️ "Furahini katika Bwana siku zote; tena nasema, furahini" (Wafilipi 4:4). Laiti kama tungeweza kusikia kusifiwa kwa Mungu zaidi kukiendelea kutoka katika mioyo yenye shukrani. Tunahitaji wakristo ambao wataendelea kuishi nuruni kila wakati, ambao wanaweza kumsifu Mungu kwa kila hali. Kwa tumaini na uhakika ambao tumeahidiwa na Kristo, tunawezaje kutokuwa na furaha?

▶️ *Hakuna kisingizio au uhalali kwa Mkristo yeyote kukatiliwa mbali. Kamwe usitoe maoni kwamba umekatishwa tamaa na njia ambayo Kristo amekuchagulia wewe kuifuata. Tabia zetu zinapaswa kubadilishwa katika sura ya Kristo. Kwa matendo na katika kweli tunapaswa kukubaliana na sheria ya Mungu. Ndipo anaweza kuonesha kupitia kwetu Baraka ambazo zinakuja kupitia kwa utii wa kanuni za neno lake. Mfalme wa mbinguni yupo tayari kumtambua mtu mnyenyekevu anayemtumikia.*

*MWENYEZI MUNGU ATUBARIKI SOTE*

No comments