AMKA NA BWANA LEO 20/10/2021

*KESHA LA ASUBUHI.*

Jumatano, 20/10/2021.

*JINSI YA KUKABILIANA NA KUFIWA.*

*Ina thamani machoni pa Bwana mauti ya wacha Mungu wake. Zaburi 116:15.*

▶️Siwezi kuelezea kwa undani ugonjwa wa mume wangu. Niliambiwa hakuwa sawa. Daktari aliniambia ingekuwa vyema kwangu kama ningemwona. Walinipeleka chumbani mwake na pindi tu nilipomtazama, nilisema, "Mume wangu anakufa." Kulikuwa na mwonekano wa kifo katika uso wake. Nilishtushwa sana. Nilipiga magoti pembeni mwa kitanda chake. Nilimwomba Mungu kwa kina sana ili asije akafa....

▶️Nilikuwa pamoja naye usiku wote, na siku iliyofuata wakati wa mchana alikuwa na ubaridi na tangu wakati huo hakuweza kuhisi chochote. Alipumzika.... Tuliwapigia simu Willie na Mary waje.... Katika juma moja tangu kifo chake Willie na Mary walikuja; pia John White [kaka yake na James White, Mchungaji wa Kimethodist].... 

▶️John White akasema, "Ellen, ninasikitika sana kukuona ukiwa dhaifu. Jaribu kubwa liko mbele yako katika huduma ya mazishi kesho. Mungu akusaidie, dada yangu mpendwa, Mungu akusaidie katika tukio hili." Ndipo niliposema, "Kaka John, haunifahamu mimi. Kadiri hali inavyozidi kuwa ngumu, ndivyo ninavyozidi kuwa na ujasiri. Sitaruhusu kulia kwa sauti, kama moyo ukiwa umehuzunishwa. Ninamtumikia Mungu, sio kwa mhemko, bali kwa akili. Ninaye mwokozi ambaye atakuwa msaada ulio karibu nami wakati wa taabu. Mimi ni Mkristo. Ninamjua yeye ninayemwamini. Anategemea kutoka kwangu kujisalimisha kikamilifu bila kuyumba. Kuomboleza kupita kiasi hakumpendezi Mungu. Nauchukua msalaba wangu niliowekewa na ninamfuata Bwana kikamilifu. Sitajitia katika maombolezo pasi na mpaka. Sitaruhusu kuwa na hali ya hisia mbaya na ya kusononeka. Sitalalamika wala kunung'unika dhidi ya mapenzi ya Mungu. Yesu ni Mwokozi wangu. Yu hai. Hataniacha wala kunipungukia."

▶️[Siku iliyofuata,] baada ya mzee [Uria] Smith kutoa hotuba ya mazishi, ilinichukua muda kusema kitu kuwafanya wote wajue kuwa nilikuwa na tumaini la Kikristo na liliniimarisha katika saa ile ya huzuni, lakini nilihofu kuwa nisingeweza kusimama kwa miguu yangu. Hatimaye nilidhamiria kujaribu kusimama na Bwana aliniwezesha. Dakitari [J.H. Kellogg) alisimama tayari "kunishikilia," alisema, kama nikianguka....lakini niliendelea kusema kile nilichokusudia kusema kwa ufanisi...

▶️ *Nimejawa na shukrani kwa Mungu kwa kuwa sikuachwa kutafuta faraja yangu katika urafiki wa ulimwengu.*

*MUNGU ATUBARIKI SOTE.*

No comments