AMKA NA BWANA LEO 19/10/2021

*KESHA LA ASUBUHI*

 *Jumanne, Oktoba 19, 2021* 

*MAJI YALETAYO UZIMA*

_Yesu akajibu, akamwambia, kama ungalijua karama ya Mungu, naye ni nani akuambiaye, Nipe maji ninywe, ungalimwomba yeye, naye angalikupa maji yaliyo hai. Yohana 4:10._

▶️ Huu ujumbe umekusudiwa kwetu kwa hakika kama kwa mwanamke Msamaria. Unatujia kwa sauti ya kunon'gona kutoka kizazi hata kizazi, “Kama ungalijua karama ya Mungu, naye ni nani akuambiaye, nipe maji ninywe, ungalimwomba yeye, naye angalikupa maji yaliyo hai.” Zingatieni hili mioyoni mwenu. Kila roho inapaswa kuamsha ufahamu wake wa hitaji lake la kiroho....

▶️ Ni watu wengi jinsi gani ambao hawaijui karama ya Mungu. Wanaongea kuhusu ukweli, wanazungumza habari za mbinguni na za dini, wanaiongelea Imani, lakini hawaifahamu. Hawana ufahamu wa uzoefu wa imani, au inamaanisha nini kumwamini Mungu, ambao ni kuyanywa maji ya uzima kila siku maishani.

▶️ Je! Kuna yeyote.... Ambaye ana kiu ya maji ya uzima, na kuhisi – yaani, laiti kama ningeyapata? Natazama kulia, hayapo, nayatafuta upande wa kushoto, siyaoni. Natazama mbele yangu, na nyuma yangu, na bado simwoni Mwokozi wangu. Je! Unataka kufahamu jinsi ya kumpata? Njoo kwake kama mhitaji na mtegemezi jinsi ulivyo, katika unyenyekevu wa mtoto mdogo, katika ujasiri wote kama ule alionao mtoto kwa wazazi wake, na mwombe Mwokozi akuhurumie katika hitaji lako kuu. Mwambie kuwa unahitaji maji ya wokovu....

▶️ Kama tusipokunywa maji ambayo Kristo anatoa, hatuwezi kuboresha hali yetu au ya wale walioko karibu nasi. Ni kwa kugawiwa tu ile neema ambayo Yesu Kristo hutupatia na anatamani kutupatia, ndipo mahitaji ya roho zetu zilizo tayari kuangamia yatatimizwa.

🔘 *Mwanamke huyu kuwa Msamaria haikuwa sababu ya kutokumjua Yesu Kristo, kwa kuwa alikuja kuwaokoa Wasamaria kadhalika na Wayahudi. Kwake Yeye hakuna watu waliotupwa au waliopendelewa. Alikuja kuchukua dhambi za ulimwengu. Yuko tayari kufanya hivi kwa wote, Wayahudi au Wamataifa, na hili lazima tulifanye kabla hatujaingia mbinguni.

No comments