AMKA NA BWANA LEO 17/10/2021
*KESHA LA ASUBUHI.*
Jumapili, 17/10/2021.
*DINI YA MANENO MATUPU.*
*Na kama ukimkunjulia mtu mwenye njaa nafsi yako, na kuishibisha nafsi iliyoteswa; ndipo nuru yako itakapopambazuka gizani; na kiwi chako kitakuwa kama adhuhuri. Isaya 58:10.*
▶️ Kuna uzoefu wa uongo ambao umeenea sana kila mahali kuhusu upendo wa Yesu — kwamba inatupasa kukaa katika upendo wa Kristo, kwamba kumwamini Yesu tu inatosha - lakini hizi roho lazima zifahamishwe kuwa upendo wa Yesu moyoni utaongoza katika maisha ya unyenyekevu na utii kwa amri Zake zote. "Yeye asemaye, nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake" (Yohana wa kwanza 2:4). Upendo wa Yesu ambao hauendi mbali zaidi ya midomo hautaokoa roho yoyote, bali kuwa udanganyifu mkubwa. - Manuscript 26, October 17, 1885,, "First Visit to Sweden, diary."
▶️ Baadhi ya wale wanaodai kumpenda Yesu ni waongo na dini yao ni ya maneno matupu. Haiwezi kubadili tabia. Na haiwezi kudhihirisha utendaji wa neema ndani yao. Wala hawaoneshi kuwa wamejifunza katika shule ya Kristo masomo ya Upole na unyenyekevu wa moyo. Hawawezi kuonesha kwa kuishi au kwa mwenendo kwamba wamejitia nira ya Kristo au kuichukua mizigo ya Kristo. Hawawezi kukifikia kiwango walichopewa katika Neno la Mungu, bali kiwango cha wanadamu. Maisha yao sio safi kama maisha ya Kristo. Hawawezi kusafishwa na kufanywa upya kwa Roho Wake. Hawakuijua njia ya Kweli, na ni miongoni mwa wale watakaosema, "Bwana, Bwana, utufungulie. Tumefundisha mitaani. Tumefanya miujiza mingi." Lakini Kristo atawaambia, "Sikuwajua ninyi kamwe, ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu" (Mathayo 7:23). - Ibid.
▶️ *Wale wanaoukataa ukweli wa Biblia wanafanya hivyo wakijidai kumpenda Yesu. Wale wanaompenda Yesu wataudhihirisha upendo huo kwa kuwa watoto watiifu. Watakuwa watendaji wa neno na sio wasikilizaji tu. Hawatakuwa wakidai kila wakati, "Kile chote tunachopaswa kufanya ni kumwamini Yesu." Huu ni ukweli katika ukamilifu wake, lakini hawawezi kuelewa, wala hawauchukui katika uhalisia wake. Kumwamini Yesu ni kumchukua kama mkombozi wako, kama mfano wako. Wale wote wanaompenda Yesu imewalazimu kufuata mfano wake. Imewapasa kujishikamanisha na Yesu kwa karibu sana kama vile tawi linavyokuwa limeunganishwa na mzabibu ulio hai. Wanakaa ndani ya Yesu na Yesu anakaa ndani yao na ni watendaji Neno Lake, washirika wa asili yake ya uungu. - Ibid.*
*MUNGU ATUBARIKI SOTE.*
Post a Comment