AMKA NA BWANA LEO 12/10/2021
*KESHA LA ASUBUHI.*
Jumanne, 12/10/2021.
*USIJITENGE NA MSALABA.*
*Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini? 2 Wakorinto 6:15.*
▶️Katika maono ya mwisho kupewa, nilionyeshwa kwamba ulikuwa na shauku ya kuwa watoto wako wangekuwa na dini imara ambayo itawafanya wakubaliwe na wote, bila ya kukosolewa na yeyote. Ushawishi wa Roho wa Mungu umewabadilisha lakini kidogo....
▶️ Pale tunapokiri kuwa watumishi wa Kristo, inatupasa tusiendelee kuutumikia ulimwengu, haitupasi kuwa na umoja au ushirika na wale wanaoukataa ukweli ambao tunauona kuwa mtakatifu. Nilielekezwa kwa Yohana wa kwanza 2:6. "Yeye asemaye ya kuwa anakaa ndani yake, imempasa kuenenda mwenyewe vile vile kama yeye alivyoenenda." "Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu. Mimi ni mzabibu, ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lolote" (Yohana 15:4,5)....
▶️ Hamwezi kujipima kwa vipimo vya kidunia au kwa maoni ya watu wengine. Usalama wenu pekee ni kuulinganisha msimamo wenu na kile ambacho kingekuwa msimamo wenu endelevu kwenda mbele na kuelekea juu tangu mlipokiri kuwa wafuasi wa Kristo. Tabia yako ya maadili inapita ikichunguzwa mbele za Mungu. Unapimwa kwa mzani wa patakatifu, na, ikiwa hali yako ya kiroho hailingani na hadhi na fursa ulizopewa, unaonekana umepungua. Njia yako ilipaswa kuendelea kung'aa na angavu, na uzae matunda mengi kwa utukufu wa Mungu.
▶️ Umepungua, unatulia bila kujali na umeridhika mno kana kwamba wingu lilitangulia mbele yako mchana na nguzo ya moto usiku kama ishara za neema ya Mungu. Mnajihesabu wenyewe kuwa miongoni mwa wateule, watu wa pekee wa Mungu, na bado hamna udhihirisho au uthibitisho wa uweza wa Mungu wa kuokoa kabisa. Hamjatengwa na ulimwengu kama vile Mungu atakavyo watu wake watengwe....
▶️ *Watu wa Mungu wako katika vita ya kila siku ili kudumisha tabia yao ya pekee na takatifu, na hakuna hali au mazingira yoyote ambayo yapasa msalaba wa Kristo kuepukwa au kuwekwa kando.*
*MUNGU ATUBARIKI SOTE.*
Post a Comment