AMKA NA BWANA LEO 08/10/2021
*KESHA LA ASUBUHI*
Ijumaa, Oktoba 8, 2021
*YAFIKIRINI YALIYO JUU*
_Yafikirini yaliyo juu, sio yaliyo katika nchi. Kwa maana mlikufa na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu. Kristo atakapofunuliwa, aliye uhai wetu, ndipo na ninyi mtafunuliwa pamoja naye katika utukufu._ Wakolosai 3:2-4.
📖 Tunahitaji kuwa na mtazamo mpana wa Mwokozi kama “Bwana na Kristo." "Nguvu zote" amepewa yeye ili kuwapatia wale wote wanaodai kuliamini jina lake. Tumeshindwa kumwonesha hata nusu ya haki yake kwa heshima yetu na utii, na kwa imani yetu inayoongezeka kwake....
📖 "Vaeni basi, kama wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao," mtume anaendelea, "moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu, mkichukuliana na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi.
📖 "Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu. Na Amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu, ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukurani. Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na tenzi, na nyimbo za rohoni, huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu" (Wakolosai 3:12-16)
📖 Hebu jiweke chini ya nidhamu ya Kristo. Kubali kuongozwa na neno lake. Zingatia maagizo yake, "Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo: nanyi mtapata raha nafsini mwenu" (Mathayo 11:29).
📖 Nayasihi makanisa kila mahali kufanya kazi kamilifu ya umilele kwa kutubu na kuachana na dhambi. "Kwa kuwa uweza wake Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa" (2 Petro 1:3). Kwa njia gani? “Kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe." "Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo toka utukufu hata utukufu" (2 Wakorintho 3:18).
🔘 *Mungu na Kristo pekee ndio wanaojua ni nini gharama ya roho za watu. Kwa ajili yetu mwana wa Mungu alifanyika kuwa masikini, ili kwamba kwa umasikini wake sisi tupate kuwa matajiri kwa utajiri wa uzima. Upendo wake hauna mfano.*
*MUNGU AKUBARIKI SANA*
Post a Comment