AMKA NA BWANA LEO 07/10/2021
*KESHA LA ASUBUHI*
Alhamisi, Oktoba 07, 2021
*NGUVU ZA KUPATA USHINDI*
_Bali mtakaseni Kristo Bwana mioyoni mwenu: muwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu lakini kwa upole na kwa hofu._ 1 Petro 3:14,15.
📚 Katika nyakati ambazo tunaishi sasa kuna hitaji la wasaidizi wa nafsi kamilifu. Tabia inayofaa ya mafundisho tunayoyakiri italeta mvuto katika mioyo, kwa kuwa wajumbe wa mbinguni hushirikiana na mtendakazi ambaye imani na matendo yake vimeunganishwa. Yeye ambaye ana uhusiano mahususi na Yesu Kristo, atakuwa na ushuhuda wa kutoa kama ushahidi kwa Bwana. “Ninyi mmekuwa rafiki zangu,” alisema Kristo, "mkitenda niwaamuruyo" (Yohana 15:14).
📚 Wale wote ambao kwa kweli ni marafiki wa Kristo watazifanya kazi za Kristo. Tuna mwelekeo wa kuleta tabia isiyotakaswa, isiyoongoka katika serikali ya familia zetu na ndani ya kanisa, na haya huyafanya maneno yetu, tabia zetu, na roho zetu, sio kosa tu nyumbani, lakini pia kwa kanisa na katika ulimwengu wote wa mbinguni. Mungu huiita roho iliyopotoka.
📚 Ikiwa wote wangeweza kuona jinsi Mungu anavyoichukulia tabia ya ubinafsi, ya kijinga, wangejidharau kabisa, na wangefanya juhudi zilizokusudiwa kuondoa kutoka kwao kila tendo lisilofaa. Wazo kwamba wanadamu wanaweza kuungana na familia ya Mungu wakiwa na tabia zisizokubalika na zisizobadilika katika maisha haya ni udanganyifu na mkanganyiko mkubwa.
📚 Nguvu ya kushinda hutegemea, sio katika mazingira, sio kwa mtu yeyote anayeishi, hata awe amesoma kiasi gani, bali katika msaada uliopo ambao Mungu hutupatia. Ukweli sio kitu cha kutunzwa kwa kufungiwa kwenye chupa kwa hafla za faragha. Ikiwa ukweli uko moyoni mpokeaji atadhihirisha imani ile ifanyayo kazi kwa upendo, na kuitakasa nafsi. Kanuni zake za kudumu moyoni zitaonyeshwa kila wakati na katika hafla zote....
🔘 *Mafanikio yetu yote, ufanisi wetu wote, uko katika Kristo. Inatulazimu tuangalie juu zaidi ya msaada wa kidunia, juu zaidi ya nguvu kubwa ya mwanadamu, juu zaidi ya mitume. Inatulazimu kuifunga imani yetu moja kwa moja juu ya Kristo mwenyewe. Ametangaza, "Pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lolote" (Fungu la 5). "Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu" Fungu la 4).*
*MUNGU AKUBARIKI SANA*.
Post a Comment