AMKA NA BWANA LEO 03/10/2021

*KESHA LA ASUBUHI*

Jumapili, Oktoba 03, 2021

*NGUVU YA NEEMA IBADILISHAYO*

_Ikawa alipokuwa mahali fulani akiomba, alipokwisha, mmoja wa wanafunzi wake alimwambia, Bwana tufundishe sisi kusali, kama vile Yohana alivyowafundisha wanafunzi wake._ Luka 11:1

📖 Kila roho ina fursa ya kueleza kwa Bwana mahitaji yake maalum na kutoa shukrani zake binafsi kwa baraka ambazo huzipokea kila siku. Lakini sala nyingi ndefu na zisizo na roho na imani ambazo hutolewa kwa Mungu badala ya kuwa za kufurahisha kwake, zimekuwa mzigo. Tunahitaji, tena, sana mioyo safi iliyobadilishwa. Tunahitaji kuimarishwa kwa imani yetu kila siku. "Ombeni, nanyi mtapewa," Mwokozi aliahidi; "tafuteni, nanyi mtaona; bisheni nanyi mtafunguliwa" (Mathayo 7:7). Tunahitaji kujifunza kuamini neno hili, na kuleta nuru na neema ya Kristo katika kazi zetu zote. Tunahitaji kumshikilia Kristo, na kuendelea kumng'ang'ania hadi tujue kwamba nguvu ya neema yake ibadilishayo inadhihirishwa ndani yetu. Inatulazimu kumwamini Kristo kama tunataka kuakisi tabia ya uungu.

📖 Kristo aliuvika uungu wake kwa ubinadamu, na aliishi maisha ya maombi na kujikana nafsi, na ya kupambana kila siku na majaribu ili kwamba aweze kuwasaidia wale wote ambao leo hushambuliwa na majaribu. Yeye ndiye ufanisi na nguvu zetu. Anatamani kwamba, kupitia matumizi ya neema yake, ubinadamu ushiriki asili ya uungu.... Neno la Mungu katika agano la kale na jipya, kama likisomwa kwa uaminifu na kupokelewa maishani, litatoa hekima ya kiroho na kimaisha. Neno lake linapaswa kupendwa sana. Imani kwa neno la Mungu na katika nguvu ya Kristo kubadilisha maisha itamwezesha anayeamini kuzifanya kazi zake, na kuliishi neno na kuwa na maisha ya furaha katika Bwana. 

📖 Tena na tena, nimeagizwa kuwaambia watu wetu, "Ruhusu Imani yako na tumaini lako liwe kwa Mungu. Usimtegemee mwanadamu yeyote anayekosea kukufafanulia majukumu yako." ...Ni vyema kwamba ndugu washauriane, lakini, wakati watu wanapanga tu kile ambacho ndugu zao watafanya, hebu na wajibu kwamba wamemchagua Bwana kuwa mshauri wao....

🔘 *Hakuna nguvu kwa mtu yeyote kurekebisha tabia hiyo yenye kasoro yeye binafsi. Tumaini na imani yetu lazima viwe katika mmoja aliye zaidi ya mwanadamu. Tunahitaji kila siku kukumbuka kwamba msaada wetu umewekwa kwa mmoja ambaye ni mwenye uweza. Bwana ametoa msaada unaohitajika kwa kila roho itakayoupokea.*

*MUNGU AKUBARIKI SANA*

No comments