AMKA NA BWANA LEO 02/10/2021
*KESHA LA ASUBUHI*
Jumamosi, 02/10/2021.
*KUWA MWANAMGAMBO WA MUNGU.*
*Wala msiifuatishe namna ya dunia hii, bali mgeuzwa kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu. Warumi 12:2.*
▶️ Inatulazimu kujikomboa kutoka kwa mila na utumwa wa jamii, ili kwamba, wakati kanuni za Imani yetu zikiwa hatarini, tusisite kuonyesha rangi zetu halisi, hata kama tutasondwa vidole kwa kufanya hivyo. Dumisha dhamiri yenye huruma, ili uweze kusikia mnong'ono wa sauti ndogo inayoongea kwa namna ambayo mwanadamu hajawahi kuongea. Hebu wale watakaoivaa nira ya Kristo waoneshe kusudi lisilobadilika la kufanya ilivyo sahihi kwa sababu hiyo ndiyo haki. Kaza jicho lako kwa Yesu, huku ukiuliza kwa kila hatua, "Je! Hii ndiyo njia ya Bwana?" Bwana hatamwacha mtu yeyote anayefanya hivi kuwa lengo la majaribu ya shetani.
▶️ Wakati mashaka yanapotokea, kama ambayo kwa hakika hutokea, mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Na kisha, wakati adui anapowajia kama gharika, Roho wa Bwana atainua viwango vyenu vya maadili. Dhamiria kuwa kuna kazi kubwa inayopaswa kufanyika, na kwamba hakuna ushawishi wa mtu au upinzani utakao kuhamisha kutoka kwenye njia wazi ya uwajibikaji. Basi unaweza kusema na Nehemia, "Mkono wa Mungu wangu U mwema juu yangu" (angalia Nehemia 2:18)
▶️ Wakati watu waliounganishwa na kazi ya Mungu wanapojiruhusu kununuliwa na kuuzwa, wanapokiuka ukweli ili kupata kibali na idhini ya watu, Mungu huwanakili katika kitabu chake kama wasaliti wa amana takatifu. Hebu kila mtu asimame katika uhuru wa maadili, akiwa ameamua kwamba akili yake itafanywa upya na Roho Mtakatifu. Mungu anawaita watu thabiti, wasio tayari kusema maneno ya wanadamu ambao, kama wakiwa wangebadilishwa wangeweza kuwa na ushawishi mzuri, lakini wakiwa hawajabadilishwa, hawawezi kutegemewa. Katika wakati wa dharura wana uhakika wa kuelekea katika njia za uongo. Bwana asingependa tumuige mtu yeyote, lakini tufuate hatua kwa hatua kumjua yeye....
▶️ *Hatupaswi kujitengeneza kwa kigezo cha ulimwengu au kwa kufuatisha namna ya ulimwengu. Watu wa Mungu watasikia mazungumzo kuhusu utekelezaji wa mbinu na mipango mibaya. Maneno ya kishenzi yataongelewa. Dini itadhihakiwa. Sikia sauti ya Mungu, "Mwanangu, wenye dhambi wakikushawishi, wewe usikubali" (Mithali 1:10). Wale ambao walitawaliwa na Roho wa Mungu wanapaswa kuweka macho uwezo wa fahamu zao.... Kuwa na ujasiri wa kutenda haki. Ahadi ya Mungu ni ya thamani kubwa kuliko dhahabu na fedha kwa wote ambao ni watendaji wa neno lake. Hebu wote waichukulie kama heshima kubwa kutambuliwa na Mungu kama watoto wake.*
*MUNGU ATUBARIKI SOTE.*🙏
Post a Comment