RAIS WA KOREA KUSINI APIGA MARUFUKU ULAJI WA MBWA
Moon Jae-in rais wa Korea kusini ametoa dokezo la kuweka sheria ya kukataza ulaji wa Mbwa nchini mwake baada ya wanaharakati za haki za wanyama Duniani kuzidi kulisonga taifa hilo, Uchina na Korea kaskazini katika kile kinachoitwa kutozingatia haki za wanyama.
Takwimu zinaonesha Korea kusini kwa mwaka
huchinja zaidi ya MBWA milioni moja kwa ajili ya
kitoweo na ndio nyama pendwa zaidi nchini humo
ikifuatiwa na Nguruwe.
Moon Jae-in ni moja kati ya watu ambao wanahusudu ulaji wa nyama hiyo lakini kwa taarifa ya jana iliyotolewa na BBC anasema wakati umefika kwa kupitisha sheria ya kuwalinda wanyama hao pamoja na Paka.
Post a Comment