MATUMIZI YA TAKWIMU BADO NI CHANGAMOTO NCHINI
Waziri wa Afya Mendeleo ya Jamii jinsia Wazee na Watoto Dkt Dorothy Gwajima amesema kuwa matumizi ya takwimu zenye ubora katika halmashauri nchini bado ni changamoto hali ambayo inarudisha nyuma sekta ya afya.
Hayo ameyasema September 7,2021 wakati wa madhimisho ya siku ya Epidemiology Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere square Dkt.Gwajima amesema kuwa ili kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji wa magonjwa na matukio yanayoathiri afya ni vema kutambua mapema viashiria hatari.
“Katika jamii yetu ni lazima pawepo na takwimu zenye ubora katika ngazi ya halmahauri jambo litakalo saidia kuinua sekta ya afya, ” amesema Dkt Gwajima
Aidha, Dkt.Gwajima ameeleza kuwa jumla ya watumishi 512 kutoka idara ya afya ya binadamu na idara ya afya ya mifugo wamepatiwa mafunzo katika ngazi ya kozi ya awali kutoka mikoa yote 26 na halmashauri 159 kwa kipindi cha miaka sita.
Kwa wake MKurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya Dkt.Leonard Subi amesema zaidi ya watanzania 512 wamepatiwa mafunzo ya utaalam wa epidemiolojia na maabara katika mikoa yote 26 Tanzania
Madhimisho ya siku ya Epidemiolojia yamefanyia kwa mara ya kwanza nchini Tanzania kuadhimishwa siku ya wataalamu wa epidemiolojia na maabara ambao ndiyo makachero wa magonjwa yote ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza ili kutambua visababishi vya magonjwa na jinsi magonjwa yanavyo sambaa kwenye jamii .
Hata hivyo madhimisho hayo yamebebwa na kauli mbiu isemayo kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji wa magonjwa na matukio yanayoathiri afya ili kutambua viashiria hatari kwa jamii.

Post a Comment