MAMA AJIFUNGUA KARUNGUYEYE SIMIYU

Katika hali isiyokuwa ya kawaida Mwanamke mmoja, Regina Frednand (46) mkazi wa mtaa wa Butiama kata ya Sima Halmashuari ya Mji wa Bariadi amezua taharuki baada ya kudai kuwa amejifungua mnyama aina ya Karunguyeye badala ya Binadamu kama ilivyozoeleka.

Akiongea na Waandishi wa Habari waliofika nyumbani kwake jana na kukuta umati wa watu ambao walifika kushuhudia tukio hilo, Regina amesema tukio hilo lilitokea Jumapili Septemba 12, 2021.

Regina amesema kuwa majira ya saa 1 na dakika 10 asubuhi wakati akijiandaa kwenda kwenye ibada ya kwanza kanisani, ghafla alijisikia maumivu makali tumboni na ndipo akaelekea chooni kujisaidia.

“Baada ya kufika chooni huku nikiwa na maumivu makali, haja ambayo nilikuwa nikisia haikutoka...cha kushangaza nilisikia maumivu makali sehemu za siri na kuhisi kuna kitu kinaning’ata.

“Kadri maumivu yalivyoongezeka nikajisikia kusukuma ndipo kikatoka kitu ambacho sikukielewa…nikapiga kelele kuomba msaada kwa watoto wangu ambao naishi nao hapa, baada ya kufika walikitazama na kubaini kuwa alikuwa panya buku, baadaye wakakimwagia maji ya baraka ndipo kilipogeuka na kuwa mnyama aina ya Karunguyeye,” amesema Regina.

Hata hiyo alipoulizwa kama alikuwa mjamzito, Regina alikiri kuwa alikuwa na ujauzito wa miezi mitano ambao aliupima mwenyewe nyumbani kwa kutumia kipimo cha mkono alichonunua duka la dawa (Urine Test).

Hata hivyo Regina mbali na kudai kuwa alikuwa na ujauzito, lakini hakuwahi kwenda kliniki kwa madai kuwa alikuwa anasubiri ujauzito ufikishe miezi sita ndipo tukio hilo lilitokea kabla ya kuanza kliniki.

“Baada ya tukio kutokea nikawaita ndugu na wazazi wangu waje kushuhudia ambalo lilikuwa la ajabu, Jumatatu yake nilijisikia vibaya nikaamua kwenda hopsitali ya Wilaya Somanda kwa ajili ya vipimo.

“Nilifika hospitali nikawaeleza tukio zima, kisha nikafanyiwa kipimo cha mionzi (Utlrasound) na majibu ya kipimo hicho yalionyesha hapakuwa na kitu chochote," amesema Regina.

Download Application yetu play store 👉📱

No comments