KESI YA MHE. FREEMAN MBOWE YAFIKIA PAZITO

Ata hivyo, Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi ilianza kupokea ushahidi kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Ramadhani Kingai katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu.

Kamanda wa polisi ni miongoni mwa mashahidi katika keshi hiyo, mashahidi wengine ni pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz.

Wengine ni maofisa wa polisi kutoka makao makuu ya jeshi hilo vitengo vya makosa ya kimtandao, uchunguzi wa silaha na uchunguzi wa maandishi na wengine kutoka mikoani.

Mashahidi wengine ni maaskari kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), akiwamo Luteni Denis Leo Urio kutoka Kikosi cha Jeshi cha Makomandoo, 92 KJ Ngerengere, mkoani Morogoro.

Pia wamo maofisa wa sheria kutoka kampuni za huduma za simu za mkononi za Mic Tanzania Ltd (Tigo) na Aritel.

Ata hivyo, Upande wa utetezi katika kesi ya kula njama na kutoa fedha kwa ajili ya kusaidia vitendo vya kigaidi inayomkabili, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu, walipinga maelezo ya onyo yaliyotolewa na shahidi kwa kwanza katika kesi hiyo, yasipokelewe kama kielelezo na Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, kwa sababu yamechukuliwa nje ya muda.

Maelezo hayo yametolewa leo Jumatano, 
Septemba 15, 2021 na Kamanda wa Polisi Mkoawa Kipolisi  Kinondoni, ACP Ramadhani Kingai wakati akitoa ushahidi dhidi ya washtakiwa hao.

Mawakili wa upande wa utetezi katika kesi ya kula njama na kutoa fedha kwa ajili ya kutekeleza ugaidi inayomkabili mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu wamepinga maelezo ya onyo ya mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo, Adamu Kasekwa yasitolewe mahakamani hapo kama kielelezo na Kamanda wa Polisi Kinondoni,  Ramadhan Kingai.

Hiyo ni kutokana na maelezo hayo kuchukuliwa nje ya muda kisheria na sababu ya pili ni Kasekwa kabla na wakati wa kuchukuliwa maelezo yake katika kituo kikuu cha Polisi Dar es Salam, anadaiwa kuteswa na askari polisi chini ya usimamizi wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Ramadhani Kingai.

Mapingamizi hayo yametolewa leo Jumatano Septemba 15, 2021 na kiongozi wa Jopo la mawakili 14 wa upande wa utetezi, Peter Kibatala katika Mahakama Kuu divisheni ya makosa ya rushwa na uhujumu uchumi wakati Kingai ambaye ni shahidi wa kwanza wa upande wa mashtaka alipokuwa akitoa ushahidi wake.

Katika ushahidi wake, Kingai ameieleza mahakama hiyo kuwa yeye ndio aliyehusika kuandika maelezo ya onyo kwa Kasekwa, hivyo ameiomba mahakama hiyo iyapoke na kuwa sehemu ya kielelezo katika kesi hiyo.

Ombi hilo lilipingwa na upande wa utetezi kwa madai kuwa mteja wao alihojiwa nje ya muda wa kisheria kwa sababu, Kasekwa alikamatwa Agost 5, 2020 Moshi Mmoani Kilimanjaro na alihojiwa Agosti 7, 2020, hivyo kisheria mshtakiwa anapokamatwa anatakiwa kuhojiwa ndani ya saa nne na si vinginevyo.

Kutokana na wakili Peter Kibatala kuwasilisha mapingamizi hayo, wakili wa Serikali mwandamizi, Robert Kidando amedai kuwa mapingamizi hayo yatatatuliwa na mahakama kwa kusikiliza kesi ndogo ndani ya kesi kubwa ya msingi.

Kutokana na hali hiyo, Jaji Mustapha Siyani anayesikiliza shauri hilo, ameahirisha  kesi hiyo kwa muda hadi saa nane mchana, ambapo itakuja kwa ajili ya usikilizwaji wa kesi ndogo kuhusu utaratibu wa utoaji wa maelezo ya onyo  ya Kasekwa baada ya mawakili wake kuyapinga wakidai kuwa aliyatoa baada ya kuteswa.

(4).Katika ushahidi wake, Kingai ameieleza mahakama hiyo kuwa Julai 2020 alipigiwa siku na aliyekuwa DCI, Robert Boaz alimtaka afike ofisini kwake na yeye aliitikia wito huo.

Akiwa katika ofisi hiyo, alitambulishwa kwa Luteni Denis Urio na kwamba Boaz alimueleza Kingai kuwa, Urio ana taarifa muhimu ya uhalifu na alimwambia Luteni Urio awaeleze kwa pamoja.

"Luteni Urio alitueleza kuwa kuna kundi maalumu la kihalifu linaandaliwa na Freeman Mbowe na lilikuw ana lengo la kudhuru viongozi wa Serikali na kundi hilo lilikuwa limepanga kulipua vituo vya mafuta na masoko na kukata miti na kuweka barabarani ili gari zisipite  na kufanya uporaji.”

"Luteni Urio alitueleza kuwa lengo la kufanya hivyo ni nchi isitawalike katika kuelekea uchaguzi mkuu uliokuwa unataka kufanyika na kwamba Urio alituambia kuwa Mbowe alimuomba amtafutie makondo wa Jeshi ambao wamestaafu au waliofukuzwa kazi" amedai Kingai.

Amedai kuwa vitendo hivyo nilipangwa kufanyika katika maeneo ya Moshi, Arusha, Mbeya, Dar es Salaam na Mwanza.

Shahidi huyo ameendelea kudai kuwa baada ya kupewa taarifa hiyo, Luteni Urio aliambiwa na Boaz  aendelee kushiriki katika mpango huo na ashirikiane na Polisi kwa kila kitu kinachoendelea katika mpango huo.

"Hivyo Luten Urio alitakiwa kuripoti kwangu kwa kuwa mimi nilikuwa Kamanda wa Polisi wa  Mkoa wa Arusha kwa kipindi kile na kabla sijaondoka Dar es Salaam kwenda Arusha katika kituo changu cha kazi, Boaz alinielekeza nifungue jalada la uchunguzi kuhusiana na maelezo aliyotoa Luteni Urio," amedai.

Washtakiwa wengine ni Halfan Hassan, Mohamed Lingw'enya na Freeman Mbowe

Serikali imesema kuwa itakuwa na jumla ya mashahidi saba katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu.

Mbowe na wenzake wanakabiliwa na kesi ya Uhujumu Uchumi, wakituhumiwa kujihusisha na makosa ya Ugaidi.

Kesi hiyo namba 16 ya mwaka 2021 inayosikilizwa na Jaii Mustapha Siyani katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, imeanza kusikilizwa ushahidi wa upande wa mashtaka leo Jumatano Septemba 15, 2021, huku Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni (RPC) Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Ramadhani Kingai akifungua pazia la ushahidi wa upande wa mashtaka.

Hata hivyo Mahakama imelazimika kusimamisha usikilizwaji wa kesi hiyo badala yake sasa inasikikiza kesi ndogo kuhusiana na maelezo ya onyo ya mshtakiwa wa pili, Adamu Kasekwa baada ya upande wa utetezi kuyapinga yasipokewe mahakamani kama sehemu ya kielelezo  cha ushahidi wa upande wa mashtaka.

Kiongozi wa jopo la mawakili wa utetezi, Peter Kibatala amedai kuwa maelezo hayo yalichukuliwa zaidi ya saa mbili na kwamba pia yalitolewa baada ya mshtakiwa kuteswa.

Kutokana na hali hiyo kama ilivyo kawaida Mahakama imelazimika kuendesha kesi ndogo ili kujiridhisha kama kweli maelezo hayo yalichukuliwa nje ya muda wa kisheria na kama alilazimishwa.

Wakili wa Serikali, Robert Kidando ameieleza Mahakama kuwa watakuwa shahidi saba na kwamba leo wanaye shahidi mmoja, ambaye ni Kingai ambaye anaendelea na ushahidi.

Kwa hiyo mpaka Mahakama itakapomaliza kusikiliza mashahidi hao wa Jamhuri kisha wa utetezi kisha itatoa uamuzi wa kuyakubali au kuyakataa ndipo kesi ya msingi itakapoendelea ambapo ACP Kingai ataendelea na kesi ya msingi.






No comments