• HOME
  • BREAKING NEWS
  • TAMTHILIA
  • MICHEZO
  • MATANGAZO
  • CONTACT US

BINAGO BLOG

  • Home
  • Home / Habari / JOEL AIBUKA MSHINDI, AJINYAKULIA MILIONI 10 NA GARI MPYA

    JOEL AIBUKA MSHINDI, AJINYAKULIA MILIONI 10 NA GARI MPYA

    Bisaya Raphael September 26, 2021 Habari
    Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo. Dkt, Hassan Abbasi usiku wa Septemba 25, 2021 ametoa zawadi na kufunga Shindano la Bingwa lililowaweka pamoja vijana wenye vipaji mbalimbali ndani ya jumba moja kwa siku 75.

    Shindano hili lililoandaliwa na Kampuni ya Startimes na kuoneshwa kupitia luninga ya TV3.

    Amewasihi walioshiriki wote wa shindano hilo kutumia vyema mafunzo waliyoyapata kuboresha maisha yao.

    Meneja Masoko na Mahusiano wa Star Times Tanzania Juma Sharobaro amefafanua kwamba katika kipindi chote ambacho washiriki wamekuwa kwenye jumba hilo walipata fursa ya kujifunza masuala mbalimbali kuhusu kazi zao za sanaa, namna ya kutumia vyema mitandao ya kijamii na stadi nyingine za maisha.

    Aidha, Dkt. Abbasi ameipongeza Kampuni hiyo kwa kuanzisha shindano hilo ambalo limewakutanisha vijana toka sehemu mbalimbali nchini na kuwapa fursa za kuongeza ujuzi utakaowasaidia kwenye maisha yao.

    "Nawapongeza Star Times kwa ubunifu huu wa kipekee kwani mmetoa fursa kwa vijana na nimefurahi kusikia kila mshiriki aliyetoka kwenye shindano hili aliweza kupata kitu cha kumsaidia kwenye maisha yake,” aliongeza Dkt. Abbasi.

    Kwa upande wake Meneja Masoko na Mahusiano wa Star Times Tanzania Juma Sharobaro ameishukuru Serikali kwa kuwaunga mkono huku akiongeza kuwa shindano hilo litawainua vijana kiuchumi.

    Katika shindano hili, Joel Revocatus (Photogenic) ameibuka mshindi na kujinyakulia zawadi ya fedha za kitanzania shilingi milioni 10 na gari jipya.

    Ameishukuru Serikali ya chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo kwa kutoa kipaombele katika sekta ya Sanaa.

    Related Posts

    Habari

    Post a Comment

    No comments

    Subscribe to: Post Comments ( Atom )

    KWA SHEREHE NA SEMINA KARIBU UKUMBI WA LAKE TANGANYIKA, NZEGA-TABORA

    FOOTBALL STORIES

    Follow us

    • Like on Facebook
    • Follow on Twitter
    • Follow on Instagram
    • Subscribe on Youtube

    Popular Posts

    • kusuka na unyoaji katika Biblia
      kusuka na unyoaji katika Biblia
       KAMA MUNGU ALIVYOKWISHA KUWAONYA WANAWAKE ! NDIVYO ALIVYOKWISHA KUWAONYA WANAUME PIA. BWANA YESU asifiwe!😅 Maranatha!😅🙏🏻 N...
    • Je kutoa Mahari ni sawa ktk biblia?
      Je kutoa Mahari ni sawa ktk biblia?
      *https://youtu.be/-P4s8sVq31o* 🤔🤔🤔🤔🤔 *JE NI HALALI KWA MKRISTO KULIPA MAHARI ILI AOE?????* 🤔🤔🤔🤔🤔 . . . Hebu tutazame k...
    • HII NDIO MISINGI YA KANISA LA WASABATO DUNIANI
      HII NDIO MISINGI YA KANISA LA WASABATO DUNIANI
      KANISA LA #SDA LINA MISINGI 28 AMBAYO NI 1.Neno la Mungu 2.Utatu mtakatifu 3.Mungu baba 4.Mungu mwana 5.Roho mtakatifu 6.Uumbaji...

    Labels

    Habari MICHEZO Live injili Tamthilia Kesha la Asubuhi BREAKING NEWS magazeti Matangazo Covid19 Mastaa Viongozi today's quote Lesoni leo Wimbo wa Leo barikiwa Je Wajua? KULFI Bongo Movies Stories TETESI ZA USAJILI

    Facebook

    Created By SoraTemplates | Distributed By Gooyaabi Templates