JE, MWOMBEZI WA WANADAMU MBELE ZA MUNGU NI NANI?? JE NI MWANAMKE ADHANIWAYE KUWA MARIAM AU NI YESU??



Wapenzi wasomaji! Bwana awabariki Sana🙏.
KARIBUNI katika SoMo tajwa hapo juu.

Je, ni kweli mwanamke aweza kuwa kuhani?

Biblia inasema kuwa tangu mwanzo kuhani alikuwa jinsia ya kiume. Ndo maana tunasoma habari za Musa na haruni nduguye, hawa walihudumu mbele za Bwana katika hema takatifu wakisimama Kama waombezi wa Wana waisraeli. Baada ya haruni kufa, watoto wake wa kiume waliendeleza kazi ya ukuhani wakisimama Kama waombezi wa Wana waisraeli mbele za MUNGU. Hadi kuingia katika nchi ya kanaani makuhani walikuwa ni wanaume waliotoka katika uzao wa Haruni. Kazi ya ukuhani ilimtaka mwanamume Tena rijali.
          Hakuna MWANAMKE ambaye amewahi kukabidhiwa dhamana ya ukuhani(uchungaji)  hakuna. MUNGU hajawahi kufanya hicho kituko Cha aibu. Hivyo vituko vya wanawake kuwa wachungaji vinaonekana Leo katika miisho ya hii Dunia. Ni uasi na kukiuka maagizo ya MUNGU. 
                Adamu hakuwahi kumkabidhi Hawa kazi ya kutoa kafara katika familia yake, pia MUNGU hakuthubutu kumpa Hawa kazi ya ukuhani. Kuhani zamani za biblia alipaswa awe mume wa mke mmoja Tena anayeisimamia familia yake vyema.

JE, maria aweza kuwa MWOMBEZI WA WANADAMU?? Na je, huyu 👆 kwenye picha ni mariamu?? Huyu siyo mariamu yule myahudi. Na hakuna mtu duniani aijuwaye sura ya mariamu au sura ya Yesu. Picha ya YESU tuionayo ni yesu fake Deacon yule mwingereza pamoja na waigizaji wengine walioigiza mienendo ya YESU original. Na hii picha ya mwanamke siyo ya mariamu, huu ni udanganyifu wa Roman Catholic kupumbaza watu waliotayari kudanganywa.

MWOMBEZI wetu huko mbinguni ni Nani baasi??👇👇

1Yohana 2:1 . Watoto wangu wadogo nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na Kama mtu akitenda dhambi tunaye MWOMBEZI Kwa BABA , YESU Kristo mwenye Haki. Naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu.

👉Wakatoliki🤔hili fungu la biblia huwa hawalioni kamwe.

Warumi 8:34. Ni Nani atakayewahukumia adhabu?? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; Naam, na zaidi ya hayo amefufuka katika wafu, Naye Yuko mkono wa kuume wa MUNGU, Tena ndiye anayetuombea.

👉 Wakatoliki hawalioni hili andiko???🤔

Waebrania 7:22-25. Basi kwa kadri hii YESU amekuwa mdhamini wa agano lililo Bora zaidi. Tena wale walifanywa makuhani wengi kwasababu wazuiliwa na mauti wasikae. Bali yeye ( Yesu) kwa kuwa akaa milele , anao ukuhani wake usioondoka. Naye kwasababu hii aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye , maana Yu Hai siku zote ili awaombee.

👉 Wakatoliki 🤔hili andiko pia hamlioni??

Biblia inatuambia hivi, MWOMBEZI wetu ni Yesu maana Yu Hai siku zote ili atuombee kwa BABA MUNGU. Tena amekaa mkono wa kuume wa MUNGU.

Kwahiyo sisi WANADAMU tunapaswa kumwendea Yesu kwa njia ya maombi ya unyenyekevu na kukiri makosa yetu na kuungama, naye atatusamehe na kutupatanisha kwa BABA yake.

Hatupaswi kuwaendea wachungaji, Wala mapadri Wala maaskofu Wala makasisi Wala Papa wa Roma Vatican ili kutuombea na kutupatanisha na MUNGU. Hao MUNGU hawatambui ila anamtambuwa YESU kuwa ndiye mwenye dhamana ya kutuombea msamaha kwa BABA yake.
Natoa wito kwa waumini wa Roman Catholic wote duniani, kuanzia Leo wamwendee YESU kwa unyenyekevu naye atawasamehe Bure. YESU haitaji kitubio. Msipige magoti kwenye sanamu ziitwazo za maria Wala kitu chochote, hizo ni kufuru. Wala msipige magoti kwa askofu au papa ili awasamehe, Hawa ni binadamu hawana uwezo wa kusamehe dhambi. Msipige magoti juu ya makaburi yadhaniwayo ni ya watakatifu ili msamehewe, huo ni ushirikina na umizimu, wafu hawajui lolote.
            Mhubiri 9:5👉 Kwasababu walio hai wanajuwa ya kwamba watakufa, lakini wafu hawajui lolote, Wala hawana ijara Tena, maana kumbukumbu lao limesahaulika.

Maria alishakufa. Na haijulikani alizikwa wapi na biblia haijasema kuwa ni MWOMBEZI, hilo la kumpa maria kazi ya uombezi ni fundisho la Roma ya kidini iliyoanguka. Ni fundisho la uongo, msilikubali kataeni kuanzia Sasa. 

Kristo pekee ndiye MWOMBEZI wetu na siyo vinginevyo. Leo wote tumwendee yeye YESU atupatanishe na MUNGU Baba mwenye upendo. 
Kazi ya uombezi karibia inakoma mbinguni. Ole wako! Ole wangu Kama Yesu hataniombea msamaha kwa BABA MUNGU kwaajili ya dhambi zangu🤔 kilio nitakacholia ni Cha kusaga meno ndani ya jehanam. Utajuta , nitajuta.

Waumini wa makanisa ya jumapili, msikubali kuwa maria ndiye anawaombea mbinguni, la! Si kweli. Tunaye MWOMBEZI Kwa BABA MUNGU aitwaye YESU Kristo aliye Hai. Huyu ndiye kuhani wetu mkuu anayebeba dhambi zetu zote na madhaifu yetu pia, tumwendee yeye tu naye atatusaidia. Biblia iko wazi. Asomaye na afahamu.

Bwana awabariki. Tukutane huko mbinguni siku YESU akirudi kutuhamisha hapa.

No comments