AMKA NA BWANA LEO 30/09/2021
*KESHA LA ASUBUHI*
Alhamisi, Septemba 30, 2021
*KAZI KUBWA YA KUFANYWA*
_Kwa maana baragumu ikitoa sauti isiyojulikana ni nani atakayejifanya tayari kwa vita? Vivyo hivyo na ninyi, msipotoa kwa ulimi neno lililo dhahiri, neno lile linenwalo litajulikanaje? Maana mtakuwa mkinena hewani tu._ 1 Wakorintho 14:8, 9
📖 Kuna wengi ambao wamekuwa wakingoja kusikia "sauti Fulani" ya ujumbe ambao ungekidhi dharura. Kote katika nchi yetu Bwana anazo roho nyofu, ambazo zimesimama katika mashaka…... Ujumbe unapaswa kutangazwa kwa uwezo uliotakaswa. Neno la Bwana limetamkwa. Mungul anataka mioyo na midomo iliyotakaswa. Ujumbe wa onyo unapaswa kutolewa katika miji mikubwa, na pia katika miji na vijiji. Watu walioteuliwa na Mungu wanapaswa kuwapo kazini kwa ari, wakitoa vitabu vyetu, na kusambaza nuru. Makala katika majarida yetu hayapaswi kuwasilisha ukweli kwa mtindo wa hadithi za mahaba, kwani hii inadhoofisha mvuto ambao ungepaswa kutolewa na ukweli makini kabisa ambao umewahi kutolewa kwa wanadamu wanaokufa. Yanapaswa dhahiri kuwa na "Bwana asema hivi" Ujumbe lazima urudiwe, na sababu za Biblia kutolewa, si kwa mtindo wa hadithi za mahaba, bali kwa mtindo wa Biblia. Kuna wengi ambao wanatazamia ushahidi wa dini ya kweli.
📖 Bwana anatangaza, “Ujumbe unapaswa kutolewa kwa maneno ya onyo la dhati. Hakuna kitu chochote ambacho kitazuia uwasilishaji dhahiri wa ujumbe huo kinapaswa kuingizwa katika mipango yako. Rudia ujumbe. Uovu katika miji mikuu unaongezeka. Adui ana ushawishi mkubwa juu ya watu, kwa sababu watu wangu hawakufungua mioyo yao wapate kutambua wajibu wao. Waambie watu wangu wafanye kazi yao na watangaze ujumbe. Wanapaswa kusema na kufanya kazi kwa usahili wa utauwa wa kweli, na Roho wangu atatoa mvuto mioyoni. Hebu sauti ya kweli ya onyo na itolewe. Malaika wangu atakutangulia, ikiwa utatakaswa kupitia kwa ukweli."
🔘 *Kazi kubwa inapaswa kufanywa. Ukweli unapaswa kutangazwa kwa matamshi ya wazi. Tunapaswa kufanya kazi katika utakaso wa Roho Mtakatifu, tukitembea kwa unyenyekevu mbele za Mungu. Lazima tutume wajumbe kwenda katika sehemu zote ambazo hazijafanyiwa kazi, na Bwana atavutia mioyo. Ujumbe wa malaika wa kwanza na wa pili ulienda na nguvu ya Roho, na wale ambao katika kutangazwa kwake walitembea na kufanya kazi kwa unyenyekevu walibarikiwa sana. Hebu sote tuamke, na kwa nguvu kubwa tushikilie kazi ile inayopaswa kufanywa.*
*MUNGU AKUBARIKI SANA*
Post a Comment